Baraza la Wataalamu la Iran limemchagua Mojtaba Khamenei kuchukua nafasi ya baba yake, Ayatollah Ali Khamenei, kama kiongozi mkuu mpya wa nchi hiyo, vyombo vya habari vya serikali vinaripoti.
JINSI UTEUZI WA KHAMENEI ULIVYOTANGAZWA.
Taarifa kutoka kwa Bunge la Wataalamu ilisomwa kwa sauti na mtangazaji kwenye Televisheni ya serikali:
"Licha ya hali mbaya ya wakati wa vita na vitisho vya moja kwa moja vya maadui dhidi ya taasisi hii maarufu, na licha ya kulipuliwa kwa ofisi za Sekretarieti ya Baraza la Wataalamu, na kusababisha vifo vya wafanyakazi kadhaa na wanachama wa timu yake ya usalama, hawakusita hata kidogo katika mchakato wa kumchagua na kuanzisha uongozi wa mfumo wa Kiislamu."
Mtangazaji alipaza sauti “Allahu Akbar, Allahu Akbar, Khamenei ndiye kiongozi.”
Kiongozi mpya aliyechaguliwa licha ya vitisho - Mkuu wa Usalama wa Iran
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran amelishukuru Baraza la Wataalamu kwa kumchagua mrithi wa Ali Khamenei licha ya "tishio la Trump kulishambulia kwa bomu", kulingana na mashirika mengi ya habari ya Iran.
Ali Larijani anasema "maadui" wa Tehran walidhani nchi "itakuwa katika hali ya mkwamo" kufuatia kifo cha Ali Khamenei lakini hatimaye Bunge limeendelea na uteuzi wa Mojtaba Khamenei.





0 Comments