Header Ads Widget

CRDB YAUNGANA NA POLISI MBEYA KUELEKEA 'POLICE FAMILY DAY'.




Katika kuelekea maadhimisho ya siku maalum ya familia ya Polisi Mbeya, 2026, Benki ya CRDB Mbeya imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa Jeshi la Polisi Mbeya ili kuungana na Polisi na kuwatia moyo katika kazi wanayoifanya kulinda raia na mali zao.


Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa CRDB Mbeya Harrison Andrew, amesema CRDB bank wanatekeleza kauli mbiu yao ya "ULIPO TUPO" kwa kuungana na jamii katika shughuli na matukio mbalimbali.


Amesema kuwa mara kadhaa wamekuwa wakishiriki katika mambo mbalimbali na Jeshi la Polisi ikiwemo jitihada za kuzuia na kutokomeza uhalifu hivyo kuelekea sikukuu maalum ya familia ya Polisi Mbeya watakuwepo kuungana na jamii ya wana Mbeya.




Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga, ameshukuru kwa msaada wa jezi za michezo (mpira wa miguu na riadha) zilizotolewa na Benki hiyo na kuwakaribisha wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuungana na Jeshi hilo katika Maadhimisho ya siku maalum ya familia ya Polisi Mbeya itakayojumuisha michezo mbalimbali, burudani na utoaji wa elimu ya masuala ya ulinzi na usalama.


Ikumbukwe na kuzingatiwa kuwa siku maalum ya familia ya Polisi huadhimishwa kila mwaka ambapo kwa mwaka huu inatarajiwa kuadhimishwa siku ya jumamosi februari 14, 2026 kama sehemu ya Jeshi hilo kufanya tathmini ya utendaji kazi, kutoa zawadi kwa Askari waliofanya vizuri zaidi katika utendaji kazi, kuungana na wadau mbalimbali wa ulinzi na usalama wakiwemo wananchi.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI