Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mwigulu Nchemba(Mb) leo Februari 11, 2026 amezindua na kukabidhi miundombinu ya utalii 21 iliyojengwa katika Hifadhi za Taifa za Nyerere, Ruaha, Mikumi na Msitu wa Mazingira Asilia Kilombero.
Ujenzi wa miundombinu hiyo imegharimu jumla ya Shilingi za Kitanzania billioni 114.62.
Lengo la kujengwa miundombinu hii ni kuongeza ubora wa vivutio vya utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania pamoja na kuimarisha usimamizi wa Maliasili na Utalii na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka hifadhi hizi hususani kwa kufungua shughuli za utalii ambazo zitasaidia kuleta ajira za moja kwa moja na sizizo za moja kwa moja.















0 Comments