Header Ads Widget

ANNA KILANGO "JIMBO LA SAME MASHARIKI ILI LIKUWE KIUCHUMI LINAHITAJI BARABARA YA LAMI SAME KISIWANI MKOMAZI"

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA SAME.

MBUNGE  wa Jimbo la Same mashariki wilayani Same Mkoani Kilimanjaro, Anna Kilango Malecela amesema kuwa ili jimbo hilo liweze kukua kiuchumi ni lazima barabara ya Kisiwani Mkomazi Same kujengwa kwa kiwango cha lami.



Anna ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa hadhara wa wananchi uliofanyika katika viwanja vya soko la Kariakoo kata ya Ndungu wakati akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bara, Aggrey Mwanri.

Amesema kuwa, tangu mwaka 2000 alipokuwa Mbungeni kama Mbunge wa kuteuliwa na Rais aliiomba Serikali ya awamu ya tatu, ya nne, ya tano kujenga barabara hiyo lakini alipoingia madarakani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliweza kuipitisha barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha lami

"Kwa sasa inamkandarasi mmoja amepewa fedha kidogo kidogo lakini sasa ndio amepewa Bilioni moja na milioni 500 ananza kupita kwa nguvu kuijenga barabara kwa kiwango cha lami" alisema Anna.

Na kuongeza "Hamuwezi kuona akifika haraka huku mimi nipo ndani ya kamati ya miundombinu inayojenga barabara naomba niwahakikishie barabara yenu itajengwa nitaisimamia hii barabara imepitishwa tumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan yeye ndio anaenda kutuletea uchumi wa jimbo la Same mashariki".



Mbunge huyo alisema kuwa jimbo la Same mashariki wananchi wake wanakipenda Chama cha Mapinduzi kutokana na fedha nyingi za maendeleo ambazo zimepelekwa jimbo hapo kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo jumla ya shilingi Bilioni 54.349 zimepokelewa.


Alisema kuwa, kipindi hiki alipoingia madarakani kwa awamu ya pili Januari mwaka huu jimbo hilo lilipokea kiasi cha shilingi Bilioni 44.3 kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Yongoma.


"Wananchi wa jimbo la Same mashariki ni wakulima wazuri hivyo ujenzi wa bwana hili utawanufaisha wananchi wa Maore, Ndungu na Kihurio kulima mpunga na kujipatia kipato na kukuza uchumi" alisema Anna.


Aliitaja miradi mingine ambayo imepelekewa fedha na serikali ya awamu ya sita na kiwango cha fedha kwenye mabano kuwa ni ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Amali -Malecela kata ya Kihurio,(584,280,029), ujenzi wa  kituo cha Afya Vuje (250,000,000), upanuzi wa kituo cha Afya Vunta (629,995,802).


Miradi mingine ni upanuzi wa miundombinu ya kidato cha tano katika  shule ya sekondari Misufini-Goma (389,400,000), uboreshaji wa skimu ya umwagiliaji kata ya Ndungu (6,988,082,130), ujenzi wa shule mpya ya sekondari (Mkapa) Kata ya Ndungu (584,280,029), fedha za kuchochea jitihada za maendeleo ya Wananchi (53,490,000), ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Kidaru (161,300,000), ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Msoroha  (187,300,000), ujenzi wa nyumba ya walimu 2 in 1 katika Shule ya Msingi Mgandu (100,840,907) na ujenzi wa madarasa 4 na matundu 9 ya choo shule ya msingi Kigulunde (120,378,221).


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI