Header Ads Widget

WAFANYAKAZI VIWANDA VYA CHAI NJOMBE WASITISHA MIGOMO BAADA YA KULIPWA

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio Daima Media NJOMBE

Baada ya malalamiko na migomo ya muda mrefu ya wafanyakazi wa Viwanda vya chai mkoani Njombe  kudai Stahiki zao hatimaye Kampuni ya DL Group imekiri kuwalipa mishahara wafanyakazi na Tayari  wamerejea kazini.


Septemba 5 mwaka huu katika viwanja vya sabasaba mjini Njombe wakati wa Kampeni za mgombea Urais wa CCM Dokta samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema tayari ameweka mazingira mazuri na mwekezaji.


Dr. David Langat Mwenyekiti bodi ya wakurugenzi DL Group

Baada ya Kauli hiyo ya mkuu wa Nchi Kwa mara ya kwanza Wafanyakazi wa  Kampuni hiyo kwenye Viwanda vya chai Kibena Lupembe na Luponde wamekutanana na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kampuni hiyo  Dr David Langat ambaye amesema changamoto za kusuasua kulipa wafanyakazi ilitokana na kuyumba kwa soko la chai Duniani lakini sasa amefanikiwa kulipa Stahiki zote.


Koima Langat ni Ofisa masoko wa DL Group ambaye anasema chai ya Tanzania imeonekana kuwa na ubora mkubwa Duniani hivyo wakulima Wanapaswa kuzingatia kanuni za Kilimo.


Baadhi ya wafanyakazi wa chai kibena akiwemo Neema Nchimbi na Frida Kidenya wamesema Tayari wamesitisha migomo na wanaendelea na kazi huku wakiwa na matumaini makubwa katika ustawi wa zao la chai nchini.


Zao la chai limekuwa kikwazo kwa wakulima wengi nchini kutokana na wafanyakazi kutolipwa mishahara yao kwa muda mrefu lakini kwa hatua hii huenda ikasaidia kulima chai kwa tija.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI