Na Fadhili Abdallah,
Matukio Daima Media.
Kigoma.Wananchi wa kijiji cha Maloregwa wilaya ya Kibondo wamesema kuwa ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho utawezesha upatikanaji wa huduma za uhakika za matibabu hivyo kuondoa usumbufu katuka upatikanaji wa huduma bora za afya kwenye maneo badala ya kufuatia huduma pekee ya afya iliyokuwa inapatikana katika kambi ya wakimbizi wa Burundi ya Nduta.
Ili kuanzisha mradi huo wananchi hao walilazika kuanza kuchimba msingi, kukusanya mawe.mchanga na matofali ambapo kiasi cha shilingi milioni 7.3 kilitumika ili kuanzisha mradi huo ambao kwa sasa umekamilika.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa zahanati hiyo uliofanywa na Mbio za mwenge wananchi wa kijiji hicho akiwemo Magdalena Nyungula alisema kuwa walilazimika kupata matibabu katika kambi ya wakimbizi ya Nduta na ikifika usiku upatikanaji wa huduma zimekuwa na changamoto kubwa kuingia kambini humo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha CHAUMA,Elisha Asam alisema kuwa walilazimika kuchangishana kuanza wenyewe ujenzi wa zahanati hiyo kutokana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa matibabu iliyokuwa ikiwasumbia ambapo serikali na wadau wengine walikuja baadaye na kuwaunga mkono hadi kukamilika na sasa imeanza kutoa huduma.
Akitoa taarifa ya mradi huo kwa kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Mganga Mkuu wa wilaya Kibondo,Henry Chinuka alisema kiasi cha shilingi milioni 107.3 zimetumika hadi mradi kukamilika ambapo serikali kuu imetoa shilingi milioni 77, halmashauri shilingi Milioni 265 na wanachi milioni 16.3.
Akizungumza katika uzinduzi wa zahanati hiyo Kiongozi wa Mwenge Kitaifa,Ismail Alli Ussi aliwapongeza wanachi hao kwa juhudi walizoanza kuchukua na kwamba juhudi zao zimezaa matunda kwa serikali kuu na halmashauri kuwaunga mkono na kukamilisha mradi huo.
Alisema kuwa kutekelezwa kwa mradi huo na kuanza kufanya kazi kunatokana na serikali kutekeleza mpango wa kusogeza huduma kwa wananchi ili kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote.
Mwisho.







0 Comments