Header Ads Widget

MGOMBEA UDIWANI NSALAGA AWAOMBEA KURA DK. SAMIA PAMOJA NA DKT.TULIA.




Na Josea Sinkala, Mbeya.


KATIBU wa Jumuiya ya Umoja wa vijana (UVCCM) wilaya ya Mbeya mjini, Siri Raphael, amesema Chama Cha Mapinduzi kimewaamini vijana kuingia kwenye nafasi mbalimbali za uongozi ili kuwatumikia wananchi.


Raphael amesema hayo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kampeni za mgombea udiwani kata ya Nsalaga Clemence Mwandemba ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Mbeya mjini.



Amemtaka Mwandemba kwenda kufanya kazi kwa weledi na kuwasikiliza wananchi wakiwemo wakulima na wafanyabiashara akigusia suala la kufunga biashara za watu bila utaratibu na elimu kwao mambo ambayo ameshauri kwenda kuyashughulikia kuhakikisha yanasimamiwa ikiwa ni pamoja na elimu kutolewa kabla ya wahusika kufunga maduka ya biashara za wateja.


Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM wilaya hiyo, ambaye ndiye mgombea udiwani kata ya Nsalaga, ameomba kura kwa ajili ya mgombea u-Rais wa Tanzania, mgombea ubunge wa Uyole na kata wote kupitia CCM akisema mafiga matatu yanakwenda kuibadilisha kata ya Nsalaga na Uyole kwa ujumla.


Mwandemba ameahidi kwenda kuwa sauti ya wananchi wake kwa kusikiliza kero zao kwa utatuzi wakiwemo wakulima na suala la miundombinu ya barabara akiahidi kuendelea kulivalia njuga kuhakikisha lami zinajengwa katani humo.


Wagombea mbalimbali wa nafasi za udiwani wa kata na wale wa viti maalum kutoka kata kadhaa za Jimbo la Uyole, nao wamepata nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano huo akiwemo mwanahabari Brandy Nelson Mwinuka na kuomba kura kwa CCM ifikapo Oktoba 29, 2025 uchaguzi mkuu unapotarajiwa kufanyika kote nchini Tanzania, wakiahidi CCM kuendelea kuwatumikia wananchi kwa maendeleo endelevu.

Mwisho.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI