Header Ads Widget

MADEREVA WA MAGARI WAANZA MAZOEZI GYMKHANA MOROGORO.

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro Matukio Daima.


TIMU ya Mkwawa ikiongozwa na dereva mkongwe Samir Nahdi wamenza mazoezi ya kujiweka sawa katika viwanja vya Gymkhana Morogoro ikiwa ni maandalizi ya kuhakisha wanakuwa na ushiriki katika kuelekea mashindano ya mbio za magari African Rally championship.


Wakizungumzia Maandalizi hayo Madereva hao walisema wamejiandaa vizuri na wako tayari kuonyesha ushindani mkubwa katika mashindano hayo.


Bingwa wa mashindano ya ndani Ahmed Huwel alisema yeye amejizatiti kuonesha chachu katika mashindano haya akiahidi kufanya vizuri zaidi kuliko mashindano ya ndani kwa kuwa na gari Bora na ya kisasa Africa.


"Rally hii imeandaliwa kimataifa na nzuri na itakuwa na ushindani mkubwa kwani kuna washindani kutoka nchi nyingine kama Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi na hadi India, lakini tumejiandaa vyema"alisema.


Madereva hao wakawaomba wananchi wa Tanzania na mashabiki wa mashindano hayo kujitokeza kwa wingi kuangalia mashindano hayo.


Baadhi wa wananchi wa Manispaa ya Morogoro wameeleza namna walivyojianda kuyaona mashindano hayo ambapo walisema wanaimani yataleta chachu na hamasa kwa wanamichezo ya nyanja hiyo ya magari.


Lameck Jonson alisema amekuwa akifatilia mara kwa mara mashindano ya magari kila yanapofanyika maeneo mbalimbali nchini na kuona namna yalivyo na hamasa kwa watu kujitokeza kuangalia na kwamba ya safari hii yameonyesha kuandaliwa vyema na waandaaji.


Mwisho.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI