Header Ads Widget

DC MBEYA AONYA MADEREVA WAZEMBE MAZISHI YA ASKARI ALIYEFARIKI KWA AJALI.

 

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Solomon Itunda, amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Beno Malisa kuaga mwili wa askari mwenye cheo cha Staff Sajent Felister aliyefariki kwa ajali ya gari iliyotokea akiwa kazini eneo la Iwambi Jijini Mbeya.

Tukio hilo lilihudhuriwa na familia, ndugu, maafisa wa Jeshi la polisi pamoja na wananchi mbalimbali.


Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, DC Itunda amesema Mh. Malisa ametoa pole kwa familia ya marehemu, Jeshi la Polisi na wote walioguswa na msiba huo, akibainisha kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu. 

Amesema mchango wa marehemu katika kulitumikia Taifa hauwezi kusahaulika na utabaki kuwa alama ya uadilifu na ujasiri.


Amesema ajali nyingi zinatokana na uzembe wa makusudi, ikiwemo ulevi, mwendo kasi na kutozingatia sheria za barabarani.

"Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Mh. Malisa, ameniagiza kufikisha ujumbe kuwa Serikali haiwezi kuvumilia wala kukubaliana na vitendo vya uzembe barabarani na madereva wote watakaobainika kusababisha ajali kwa uzembe watachukuliwa hatua kali za kisheria", amesema Itunda.

DC Itunda amewataka madereva wote mkoani Mbeya na nchini kwa ujumla kuwa na hofu ya Mungu, kuzingatia sheria za barabarani na kuthamini uhai wa watu.


Msiba huo pia, umehudhuriwa na Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Maduhu Kazi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI