Header Ads Widget

MASISTA WANNE WA SHIRIKA LA WAKARMELI WAMISIONARI JIJINI MWANZA WAFARIKI DUNIA.

 

NA CHAUSIKU SAID

MATUKIO DAIMA, MWANZA

Watu watano wamefariki dunia akiwemo dereva na masista wanne wa Shirika la Wakarmeli Wamisionari wa Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori wakielekea uwanja wa ndege wa Mwanza.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa, ajali hiyo imetokea Septemba 15, 2025 saa 1:50 usiku katika kijiji cha Bukumbi, Kata ya Idetemya, Wilaya ya Misungwi, barabara ya Usagara–Kigongo Feri.

Waliofariki dunia ni Mama Mkuu wa Shirika hilo duniani, Sista Nelina Semeoni (60) raia wa Italia, msaidizi wake Sista Lilian Kapongo (55) mkazi wa Tabora, Sista Damaris Matheka (51) raia wa Kenya na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Bukumbi, pamoja na Sista Stellamaris Muthin (48) raia wa Kenya. Dereva wa gari hilo, Boniphace Msonola (53), naye alifariki dunia katika ajali hiyo.

Kamanda Mutafungwa amesema chanzo cha ajali ni mwendokasi wa gari dogo baada ya kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari kisha kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa linakuja.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI