Header Ads Widget

BODABODA WAONYWA KUTOTUMIKA KWENYE UHALIFU


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2025 Ismail Alli Ussi amewataka maafisa usafirishaji wa pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda  kutotumia usafiri huo kutumika kuchochea vitendo vya uhalifu na badala yake pikipiki hizo ziwe sehemu ya kutoa ajira na kurahisisha usafiri.

Ussi alisema hayo wilayani Kasulu jana wakati mwenge wa uhuru ukianza mbio zake katika halmashauri ya wilaya Kasulu na kukabidhi mikopo ya shilingi milioni 90 kwa kikundi cha bodaboda Tushikamane Kijiji cha Kalimungoma wilayani Kasulu ambacho kimenunua pokipiki 29 kupitia mkopo huo uliotolewa na halmashauri kupitia mapato ya ndani.

Kiongozi huyo wa mbio za mwenge alisema kuwa tofauti na dhana inayojengwa kwamba waendesha bodaboda ni wahuni au wanafanya matendo ya kihuni ni vizuri kikundi hicho kuonyesha mfano kwa vitendo katika kuzitumia kutengeneza ajira lakini pia kuwa sehemu ya kuingiza kipato kwa bodaboda hao lakini chanzo cha mapato ya serikali kwa kulipa kodi na tozo mbalimbali.

Sambamba na hilo kiongozi huyo ametoa wito kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha mikopo ya uwezeshaji kwa vikundi vya vijana, wanawake na makundi maalum inayotolewa na halmashauri kupitia mapato ya ndani ni lazima na siyo hiari hivyo kila halmashauri lazima itekeleze maelekezo hayo ya serikali.

Mkuu wa wilaya Kasulu, Isack Mwakisu akizungumza wakaati akipokea mwenge wa uuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya Kibondo, Agrey Magwaza alisema kuwa ukiwa wilayani humo mwenge huo wa uhuru utakimbizwa katika halmashauri mbili za wilaya hiyo kwa umbali wa kilometa 123 ikitembelea miradi 14 yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.7.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI