Header Ads Widget

ZITTO AWATAKA WAGOMBEA UBUNGE,UDIWANI ACT KUTOKATA TAMAA.

 

Kiongozi wa Chama Mstaafu wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye ni Mgombea Ubunge jimbo la Kigoma Mjini mkoani Kigoma akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ya chama hicho eneo la Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji.


Na Fadhili Abdallah,Kigoma


 


MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini kwa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametia moyo wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho nchi nzima kuendelea na kampeni kwenye maeneo yao wakati huu uongozi wa chama ukipambana mahakamani ili kurudishwa kwa Mgombea urais wa chama hicho Mpina.


 


Zitto ambaye ni kiongozi wa chama mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo alisema kuwa kuwekewa pingamizi kwa mgombea uraisi wa chama hicho kusiwatie hofu wagombea wa ubunge na udiwani wa chama hicho  badala yake waongeze mbinu za mapambano ili waweze kushinda kwenye maeneo yao.


 


Kiongozi huyo alisema kuwa chama hicho kimeweka wagombea wanaokubalika katika majimbo na kata mbalimbali nchini ambazo zinawapa nafasi ya kushinda nafasi za udiwani na ubunge hivyo wakikata tamaa watapoteza nafasi zao bila sababu.


 


Akizungumzia ahadi za chama hicho wakipewa ridhaa ya kushika halmashauri ya manispaa Kigoma Ujiji kwa kuwa na mbunge na idadi kubwa ya madiwani alisema kuwa wataligeuza eneo la Kagera Ujiji kuwa Satelite City (Mji wa pembeni wenye huduma muhimu za kijamii) hivyo ameomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua ili kuweza kutekeleza mipango hiyo.


 


 


mgombea ubunge huyo alisema kuwa wakishinda nafasi ya ubunge na udiwani wataanzisha mpango wa hifadhi ya jamii ambao ndani yake kutakuwa na taratibu za utoaji mikopo kwa wajasiliamali na huduma za afya kwa ajili ya matiababu kwa wote




Akizungumza katika mkutano huo Mgombea udiwani kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji, Kana Abdallah alisema akichaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo jambo la kwanza itakuwa kupigania malipo ya fidia ya wananchi ambao maeneo yao yalichukuliwa na Mpango wa Uwekezaji (KISEZ) lakini malipo imekuwa na vurugu.




Mwisho.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI