Rais wa Marekani, Donald Trump ameanza rasmi ziara yake ya pili ya kiserikali nchini Uingereza siku ya Jumatano ambako amepangiwa kuwa na mazungumzo muhimu ya kidiplomasia.
Mfalme Charles na familia ya kifalme watampokea Rais Trump atakapowasili katika kasri la Windsor, eneo la zamani na kubwa zaidi kwa makazi ya Wafalme wa Uingereza kwa takriban miaka 1,000, akikaribishwa na msafara wa magari, maonyesho ya ufyatuaji risasi, maonyesho ya ndege za kijeshi na karamu ya kifahari.
Uingereza inasema itakuwa sherehe kubwa zaidi ya kijeshi ya makaribisho kwa ziara ya serikali katika kumbukumbu yake.
Trump, ameweka historia kwa kuwa kiongozi wa Marekani lakini pia mwanasiasa wa kwanza kualikwa na Mfalme wa Uingereza mara mbili.
"I Love King Charles," aliweka ujumbe huo kwenye akaunti yake ya Truth Social mnamo mwazi Februari. Aliongeza alipowasili: "Nina mambo mengi hapa ambayo ... yanauchangamsha moyo wangu. Ni mahali maalum sana."






0 Comments