Kanisa Katoliki duniani limeandika ukurasa mpya katika historia yake kwa kumkaribisha kiongozi mpya Papa Leo XIV, ambaye kabla ya kuchaguliwa alikuwa Askofu Mkuu, Robert Francis Prevost, mzaliwa wa Chicago, Marekani.
Kuchaguliwa kwake kumekuwa tukio la kihistoria lililozua shangwe, furaha, na matumaini mapya kwa zaidi ya waumini bilioni 1.4 wa Kanisa hilo duniani kote.
Katika ibada yake ya kwanza takatifu ndani ya Kanisa la Sistine, mahali patakatifu pa mafumbo na historia ya upapa, Papa Leo XIV aliongoza misa kwa unyenyekevu mkubwa, akianza kwa kukiri dhambi na kuomba msamaha wa Mungu. Kwa sauti ya matumaini na wito wa mshikamano, alisema:
"Najua ninaweza kumtegemea kila mmoja wenu kutembea nami tunaposonga mbele kama Kanisa, jumuiya ya marafiki wa Yesu, kama waumini, kutangaza habari njema, kutangaza Injili."
Lakini pamoja na matumaini haya, Papa mpya anakwenda kukutana na changamoto kadhaa. Kati ya nyingi hizi ndizo changamoto tano kubwa zinazomsubiri Papa Leo XIV katika safari yake ya kiutume.
1. Unyanyasaji wa kijinsia na watoto
Kuanzia miji ya mashambani ya Ulaya hadi barani Afrika, Kanisa Katoliki limekabiliwa na msururu wa shutuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto katika miongo michache iliyopita.
Kesi zenye ushahidi wa kutisha zimekuwa zikigonga vichwa vya habari na kuacha umma na maswali mengi juu ya suala hilo.
Uchunguzi uliokuwa na matokeo ya kuhuzunisha zaidi ulibaini kuwa watoto wapatao 216,000 nchini Ufaransa, walikuwa wametendwa vibaya kingono na washiriki wa makasisi tangu mwaka 1950.
Mnamo mwaka wa 1995, Askofu Mkuu wa Vienna, nchini Austria, alijiuzulu kutokana na madai ya unyanyasaji wa kijinsia, yaliyotikisa Kanisa.
Taarifa ya Vatican ilisema Papa Francis aliyefariki dunia Aprili 21, 2025 siku ya Jumapili ya Pasaka "alihisi uchungu" kutokana na matokeo ya uchunguzi huo, na akaelezea matumaini ya "njia ya kupatikana kwa ukombozi".
Juhudi za Papa Francis kushughulikia tatizo hilo ni pamoja na kufanya mkutano wa kilele ambao haujawahi kushuhudiwa juu ya watoto katika Kanisa, na kubadilisha sheria zake ili kuharamisha unyanyasaji wa kijinsia.
Na chini ya Papa Francis, jopo maalum liliundwa kushughulikia suala hilo lakini limekabiliwa na vikwazo, ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa viongozi wa ngazi ya juu.
Mwaka 2011, mtangulizi wa Papa Francis, Papa Benedict alitoa muongozo kupitia maaskofu kwamba taarifa zote za unyanyasaji zilipotiwe Polisi wa eneo husika badala ya kupelekwa Vaticani kama ilivyokua nyuma. Kanisa limefanya juhudi kubwa lakini minong'ono inaendelea kuhusu changamoto hii.
Papa Leo XIV atakumbana na changamoto ya madai ya kuficha suala hilo ambalo linaendelea kulichukiza Kanisa Katoliki, huku makundi ya waathiriwa wakidai kuwa Vatican haijafanya vya kutosha kurekebisha makosa yake.
2. Nafasi ya wanawake kwenye Kanisa
Kanisa linafundisha kwamba wanaume na wanawake ni sawa katika hadhi. Wito kwa utakatifu ni wa ulimwengu wote, lakini njia za kufuata hili ni tofauti.
Kuna tofauti kabisa ni katika majukumu ambayo jinsia mbili zinaweza kuwa nayo katika kujitoa kimaisha. Kwa sheria za asili, ni wanawake tu ambao wanaweza kujitoa katika maisha ya kimwili kwa kutumikia kama mama.
Kwa sheria ya kawaida, wanaume tu ndio wanaoweza kujitoa katika maisha ya kiroho kwa waaminifu kwa kuhudumu kama makuhani.
Wakati tayari Papa Leo XIV amechagulia rasmi, jukumu la wanawake kanisani ni suala zito, na kuna Wakatoliki ambao wanatumai kuwa wanawake wataweza kuchukua majukumu makubwa katika siku za usoni.
Kanisa Katoliki linakataza wanawake kuwa makuhani.
Mnamo mwaka wa 2016, Papa Francis alimteua Phyllis Zagano kwa tume ya upapa ambayo ilikutana huko Vatican kujadili ikiwa wanawake wanapaswa kuruhusiwa kuwa mashemasi.
Papa Francis aliteua wanawake wengi katika majukumu ya uongozi huko Vatican kuliko Papa yeyote kati ya waliotangulia mbele yake.
Wakati Papa Francis alikuwa wazi kutaka wanawake wapate fursa zaidi, alipinga wazo kwamba wanahitaji kuwa katika sehemu ya uongozi wa kanisa.
Mrithi wake atahitaji kuamua ikiwa ataendeleza ajenda hii au kuipatia mgongo.
3. Wapenzi wa jinsia moja
Kanisa Katoliki lilijipata katika mgawanyiko pale Papa Francis aliposema kuwa makasisi wa Kanisa Katoliki wanaweza kuwabariki wapenzi wa jinsi moja maarufu kama LGBT katika Kanisa Katoliki la Roma.
Hata hivyo, aliweka wazi kuwa baraka hazipaswi kuwa sehemu ya taratibu za kawaida za Kanisa au zinazohusiana na miungano ya kiraia au harusi na kuongeza kuwa inaendelea kuiona ndoa kuwa kati ya mwanamume na mwanamke.
Vatican ilisema inapaswa kuwa ishara kwamba "Mungu anawakaribisha wote", lakini hati iliyotolewa na Vatican wakati huo, ilisema Makasisi lazima waamue kwa kuzingatia uhalisia wa kila tukio.
Papa Francis alikosoa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja kuwa "sio haki", akisema Mungu anawapenda watoto wake wote jinsi walivyo na kuwataka maaskofu wa Kikatoliki kuwakaribisha watu wa kundi la LGBTQ kanisani.
"Mimi ni nani kuhukumu?" Papa Francis alisema wakati alipoulizwa juu ya wapenzi wa jinsi moja Julai 2013.
Ingawa Francis alikosoa kuharamishwa kwa mapenzi ya jinsia moja, aliweka wazi kuwa anaamini kwamba vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ni dhambi. "Hebu tutofautishe kati ya dhambi na uhalifu," Papa alisema.
Uamuzi huo ulikuwa wa kihistoria ambao uliwashangaza Wakristo wengi wa Kikatoliki duniani kote na karibu kwa kauli moja, maaskofu wa Kiafrika waliitikia kwa ukali fulani ambao si kawaida kwao.
Wazo hilo lilipingwa moja kwa moja katika nchi za Malawi, Nigeria na Zambia pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Katika taarifa iliochapishwa Jumamosi, Desemba 23, Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Congo (CENCO) lilikataa wazi wazi na kusema "hapana kwa aina yoyote ya baraka kwa wapenzi wa jinsi moja."
Kwa maaskofu wa Ivory Coast tamko la "Fiducia supplicans" "limepanga kuvurugika kwa watu wa Mungu".
Mwitikio sawa kutoka kwa Baraza la Maaskofu wa Cameroon. Rais wake, Bw Andrew Fuanya Nkea, aliona mapenzi ya jinsi moja kuwa ni "ugeni ambao unadhuru sana ubinadamu.
Huko Senegal, Askofu Mkuu wa Metropolitan wa Dakar, Monsinyo Benjamin Ndiaye, ndiye aliyebeba sauti ya wenzake na kusema hawapitishi "hukumu kwa watu" lakini "wanakemea mpango wowote wa kutaka kuhalalisha mapenzi ya jinsi moja..".
Suala hili ndani ya Kanisa Katoliki limezua sintofahamu. Upande mmoja kuna wahafidhina wanaokataa kubariki ndoa zisizo za kawaida na kwa upande mwingine wanamageuzi wanaodai kwamba ulimwengu na Kanisa vinaweza kubadilika.
4. Tuhuma za ubadhirifu
0 Comments