
Na Mwandishi wetu, Matukio Daima.
MGOMBEA wa udiwani kupitia Chama Chama Mapinduzi (CCM), Kata ya Lamadi, wilayani Busega Mkoani Simiyu, Joseph Goryo, amesindikizwa na mamia ya wakazi wa Mji wa Lamadi, kwenda kuchukua fomu ambapo Msafara wake ulianzia katika Ofisi za Ccm kata ya Lamadi kuelekea katika Ofisi za Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi wa kata hiyo.
Goryo tayari amechukua fomu za tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kwaajili ya kugombea nafasi ya Diwani kata ya Lamadi ambapo atachuana na vyama vingine vitakavyowasimamia Wagombea wao .
Goryo amesema kiupaumbele cha kwanza ni Fursa zinazohusiana na sekta ya Utalii na ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya ujenzi wa sokokuu la kisasa na ujenzi wa stendi ya kisasa ya Mabasi Lamadi.
Mwisho.
0 Comments