Header Ads Widget

TANZIA:MWANAHABARI TEMMY MAHONDO AFARIKI DUNIA


Mwanahabari Temigunga Mahondo amefariki Dunia Hospital ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma .


Mahondo alikuwa mwandishi wa habari na meneja wa kituo kikongwe cha Radio cha Coutry Fm cha mkoani Iringa na baada ya hapo alifanya kazi na taasisi za kimataifa za kihabari kama mkufunzi kwa wabahabari .


Mahondo pia amekuwa msaada mkubwa kwa chombo cha Matukio Daima Media kwani hadi mauti yanamkuta ndie alikuwa mkuu wa kitendo cha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi katika Matukio Daima Media .

Mahondo pindi alipolazwa Hospitali ya Mlonganzila wanakundi wa Iringa Daima ambako alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo ambalo Admin wake mkuu ni mkurugenzi wa Matukio Daima Media Francis Godwin walimchangia zaidi ya Tsh milioni 3 na yeye alitoa sehemu ya pesa hiyo kuchangia ujenzi wa ICU Hospital ya Rufaa ngazi ya mkoa ya Tosamaganga pesa alizokwenda kukabidhi mwenyewe na baadhi ya wanakundi huku akihamasisha jamii kuchangia zaidi.


Siku nne kabla ya kifo chake uongozi wa Iringa Daima ulikwenda kumtazama Hospital na kutokana na hali yake kuwa mbaya ulitangaza mchango wa dharura uliopaswa kufungwa tarehe 9/8/2025 majira ya saa 12:45 asubuhi ya jumapili tarehe 10/8/2025 wakati hamasi ya michango ikitolewa na kuongeza muda wa mchango hadi tarehe 17/8/2025  ndipo taarifa ya kifo inatolewa  na Inocent Mahondo  mdogo wa marehemu Temigunga Mahondo na kufanya mchango wa ugonjwa kugeuka kuwa wa msiba .

Temigunga Mahondo tulikupenda na tulitamani kuona unarejea salama ila Mungu kakupenda zaidi yetu hivyo Tuseme Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa jina lake na lihimidiwe😭😭
 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI