Header Ads Widget

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI: CHELSEA YAANZA MAZUNGUMZO NA LEAO

 

Chelsea wanawasiliana na Rafael Leao, Borussia Dortmund wanamtaka Jobe Bellingham na anayelengwa na Manchester City akubali kuhama Bayern Munich.

Chelsea wameanza mazungumzo ya kumsajili winga wa AC Milan Rafael Leao, huku timu hiyo ya Serie A ikiwa tayari kumruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 25 kuondoka kwa kima cha takriban £63.5m. (Caught Offside)


Arsenal imeanza mazungumzo na mlinzi wa kati wa Ufaransa William Saliba, 24, kuhusu mkataba mpya huku Real Madrid ikionyesha nia ya kumsajili. (Athletic - subscription required)

Gunners pia inakaribia kumsajili kipa wa Espanyol, 24, Joan Garcia kama wa akiba (Independent)


Kiungo wa kati wa Sunderland, Jobe Bellingham, 19, anaweza kufuata nyayo za kaka yake, 21, huku Borussia Dortmund wakipanga kumnunua kwa pauni 25m mchezaji huyo ambaye yuko timu ya England ya kimataifa ya Under-21. (Times - subscription required)


Mchezaji anayelengwa na Manchester City Florian Wirtz, 22, amekubali kujiunga na Bayern Munich, huku mabingwa hao wa Bundesliga wakiwa tayari kulipa pauni milioni 87.1 kumnunua mchezaji huyo kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani. (Bild - in German)

Rangers wanafikiria kumwajiri tena Steven Gerrard kama meneja, huku Gary O'Neil, Rob Edwards na Russell Martin pia wakizingatiwa katika nafasi hiyo. (Telegraph - subscription required)


Xabi Alonso ana nia ya kumleta mlinzi wa Bournemouth na Uhispania Dean Huijsen Real Madrid iwapo atachukua nafasi ya Carlo Ancelotti kama meneja Bernabeu. (Talksport)

Mshambulizi wa Liverpool na Uruguay Darwin Nunez, 25, ni miongoni mwa chaguzi kadhaa zinazozingatiwa na viongozi wa Serie A Napoli wanapolenga kuboresha safu yao ya ushambuliaji. (Corriere dello Sport - in Italian)

Liverpool itajadiliana na Luis Diaz, 28, kuhusu mkataba mpya msimu wa joto, huku mkataba wa sasa wa winga huyo wa Colombia ukikamilika 2027. (TBR Football).

Mmarekani John Textor amefanya mazungumzo ya kununua hisa za wenzake David Blitzer na Josh Harris na kuchukua udhibiti wa Crystal Palace , lakini anakabiliwa na ushindani kutoka kwa mmiliki wa klabu ya New York Jets Woody Johnson. (Guardian

Nottingham Forest wameungana na Newcastle na Inter Milan katika harakati za kumsajili mlinzi wa kati wa Liverpool na England Jarrell Quansah, 22. (Teamtalk).

Forest pia wanavutiwa na kiungo wa Manchester City James McAtee, lakini Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 22 pia anafuatiliwa na Tottenham na Bayer Leverkusen. (TBR Football)

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI