Header Ads Widget

BUTEMBO AREJESHA FOMU YA UDIWANI KWA KISHINDO KATA YA MAGOMENI DAR


Na. Mwandishi Wetu Dar.


MGOMBEA Mteule wa Udiwani wa Kata ya Magomeni iliyopo Manispaa ya Kinondoni kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Noordin Yusuph Hassan 'Butembo' leo Agosti 20, 2025 amerejesha fomu rasmi kwa uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

Butembo amerejesha fomu hiyo katika ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo ya Magomeni na kisha kuwatangazia umati wa wana CCM waliomsindikiza kujiandaa na kampeni za nguvu katika kusaka kura za Udiwani , Mbunge na Rais.

"Kwa sasa tukajiandae na maandalizi ya kampeni zitakazoanza rasmi Agosti 28, mwaka huu Udiwani na kumunea kura za ushindi wa kishindo  Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge kwa Jimbo la Kinondoni.



Lakini pia niwashukuru viongozi wa CCM Kata ya Magomeni katika hatua zote na sasa tunaenda kukipigania Chama nje kwa Wananchi, tuendelee kushikamana kwa pamoja " amesema Butembo.

Butembo ni kada wa CCM amekuwa Diwani wa Kata ya Magomeni kuanzia 2020-2025, na sasa anapeperusha tena bendera ya CCM kwa awamu ya pili.

Miongoni mwa mambo makubwa aliyofanya ndani ya Kata hiyo ni pamoja na kusimamia masuala muhimu ikiwemo Elimu, Afya, Mazingira na miundombinu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI