Header Ads Widget

MEZA YA MAGAZETI LEO JUMANNE JULAI 29/2025:WAGOMBEA CCM WAKESHA KUSUBIRIA MAJINA...

 

Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kikiendelea usiku huu Jijini Dodoma tarehe 28 Julai, 2025 kupitia na kuchuja mapendekezo ya majina ya wagombea wa Ubunge wa Majimbo, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Viti Maalum vya Ubunge na Baraza la Wawakilishi.

Wakati huo huo watiani CCM na wapambe na wananchi wengine wanaofuatilia mchakato hup  wamekesha wakisubiri majina kutangazwa ambapo kupitia chanel ya Matukio Daima Tv zaidi ya watu 600 walikuwepo wakisubiri .

Toka majira ya saa 11 Julai 28/2025 ambapo Matukio Daima Media na mitandao mbali mbali ilikuwa hewani kurusha matangazo hayo idadi ya watazamaji ilikuwa ni kubwa zaidi na hadi majira ya saa 10 Alfajiri bado idadi ya watazamaji walikuwepo hewani japo majina bado yalikuwa bado kutangazwa.

Hata hivyo zoezi la kutangazwa majina limepangwa kufanyika majira ya saa 4 asubuhi ya leo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI