Header Ads Widget

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI: MAN CITY JICHO KWA GUIMARAES



Manchester City wanatazamia kufufua shauku yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle na Brazil Bruno Guimaraes, 27, wakati wanajiandaa kuondoka kwa Mbelgiji Kevin de Bruyne, 33. (UOL esporte)

Chelsea wako tayari kulipa euro 120m (£102m) ili kumsajili winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 24, kama mchezaji wao nyota msimu wa joto. (Fichajes)

Manchester City wanafikiria kutoa kati ya euro 50-60m (£42-51m) kwa kiungo wa AC Milan na Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, licha ya hivi karibuni kusaini mkataba mpya hadi 2030. (Calciomercato)


Everton wanatarajia kumpoteza mlinzi wa kati wa England Jarrad Branthwaite, 22, msimu huu huku Manchester United na Tottenham zikimtaka. (Sun)

Chelsea na Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Benfica na Ugiriki Vangelis Pavlidis, 26, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Barcelona na Atletico Madrid. (Record)

Arsenal na Liverpool wanatafuta mbadala wa Alexander Isak huku Newcastle wakisisitiza kwamba hawatamuuza mshambuliaji wao wa Sweden mwenye umri wa miaka 25. (i paper)


Newcastle, Wolves na Brentford wanamtazama mlinda lango wa Angers na Ivory Coast Yahia Fofana, 24, kabla ya uhamisho wa pauni milioni 15 msimu wa joto. (Football Insider)

Chelsea wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Sunderland na England chini ya umri wa miaka 21 Jobe Bellingham, 19, mbele ya Manchester United, Arsenal, Tottenham, Brighton na Crystal Palace. (Caught Offside)

Leeds itasikiliza ofa kwa ajili ya mlinda lango wa Ufaransa Illan Meslier, 25, na kutumia fedha hizo kusajili mbadala wa chaguo la kwanza. (Football Insider)

Juventus wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, msimu wa joto, lakini wanataka karibu euro 40m (£34m). (Tuttosport)


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI