Header Ads Widget

JIMBO LA NZEGA VIJIJINI SEHEMU YA TATU



Bado tuko jimbo hili na tumechukua muda mwingi kumwelezea Dk. Hamis Kigwangalla kwa mapana na marefu hasa yale magumu ambayo ameyapitia katika uongozi wake wa kisiasa.

Tumefanya hivyo kama njia ya kiungwana, kwanza imewasaidia wasomaji wengi kuelewa na kumwelewa Kigwangalla kwa kiasi fulani hasa yale yaliyojificha au kufichwa, mazuri na mabaya.

Hata hivyo, haimaanishi kuwa tunamwelewa Dk. Kigwangalla kwa kiwango hicho, isipokuwa kwa kadiri na namna fulani.

Lakini pia, baadhi ya mambo kuhusu Dk. Kigwangalla tutayaeleza kupitia makala za jimbo la Nzega mjini ambayo tukiyaeleza katika makala haya ya jimbo la Nzega Vijijini hayataleta maana halisi kwa kuwa yanatokana na historia na mambo yaliyopo katika jimbo la Nzega mjini.

Hivyo, tuweni wavumilivu tu tutafikako.


Leo tutaeleza suala moja tuliloahidi juu ya kwa nini wana siasa wengi wanakimbilia jimbo hili la Nzega Vijijini. Kwanza kabisa niweke wazi kwamba, mtu kugombea anapotaka na nafasi yoyote ni haki yake ya kikatiba, lakini vile vile kuitumia haki hiyo kwa sababu tu fulani fulani au mashinikizo fulani ndipo hasa ilipo hoja yangu hiyo.

Kama nilivyokwisha kusema huko nyuma kwamba, Dk. Kigwangalla amechafuliwa kwa namna moja au nyingine tena kwa makusudi kabisa, na yeye kwa sababu hana visasi na kwa amekuwa akipuuzia mambo hayo, yamepelekea kuufanya uongo kuwa ndiyo ukweli na ukweli kuwa uongo.

Kwa mfano, ukiwasililiza watu tena viongozi wa chama huko vijijini, wanadai kwamba Dk. Kigwangalla hapokeagi simu ukimpigia, lakini ukiwauliza ni nani anayepokeaga simu? Wanasema Bashe anasaidia watu ila Kigwangalla hakuna.

Ukimwambia hebu mpigie simu Bashe unaona kiswahili kimekuwa kingi, hapigi simu kwa kuwa anajua ukweli hata huyo anayemaifu hawezi kupokea hiyo simu yake. 

Kuna siku hawa wapambe wa Bashe niliwahi kuwaambia, ukiondoa mambo ya mabarabara, taa za solar za barabarani, zahanati na madarasa ambayo ni wajibu wa serikali kuyafanya, watutajie mambo mawili tu ya kumsifia Bashe ambayo ameyafanya Bashe kama mbunge, halafu na mimi nitaje mambo mawili tu ya hovyo ambayo Bashe amekuwa akiyafanya kama mbunge. 

Lakini pia, wataje mambo mawili ya hovyo ambayo wanaona Dk. Kigwangalla ameyafanya, na mimi niyataje mambo mawili tu ya kumsifia Dk. Kigwangalla ambayo ameyafanya kama mbunge.

Wenzangu wakakosa hoja, wakawa wakali badala ya kujenga hoja na mjadala wetu ukaishia hapo.



Na hiyo misaada inayoongelewa kutolewa, au yale yanayosifiwa kufanywa na Bashe ni hakuna bali ni propaganda tu zilivyotengenezwa na wapambe wake. Mengi yamejificha ndani ya propaganda hizo.

Kinachomfanya Dk. Kigwangalla ashambuliwe na kutengenezewa ubaya hata ambao hana ni kwa sababu kwanza yeye hajali na hana kundi la wapambe kama ilivyo kwa Bashe, yeye Bashe huwa anakundi la wapambe ambao wanaishi kwa kutegemea upambe zaidi.

Na kama ilivyo wapambe kazi yao nikufanya upambe, bahati mbaya wapambe hao hufanya kazi ya upambe kwa kufitinisha watu, kudanganya na kulazimisha kutengeneza matukio ya kuwaumiza wengine ili waonekane wanampambania mtu sao na ili awanyoshee mkono wa chochote.

Ndiyo kazi ya wapambe wa aina hii maarufu kama "chawa".

Hili nitalifafanua zaidi tutakapoingia kujadili jimbo la Nzega mjini.

Lakini haya yote yamechangia sana wanasiasa wengi kukimbilia majimbo haya mawili, Nzega Vijijini na Bukene.

Bwana Bashe amefanya siasa za Nzega kuwa za fitina, chuki na kuumizana, ufisadi, na za kujadili wali na nyama kuliko masuala ya msingi kama mbinu na mikakati ya kuhakikisha wilaya yetu inapiga hatua kwenda mbele kimaendeleo.

Kuna mikoa au wilaya inayojulikana, kwamba suala la elimu halina vyama, zaidi ya mshikamano katika mkoa or wilaya.

Katika mikoa hiyo au wilaya, unakuta kila mtu matamanio yake anataka ajue ni watoto wangapi wamemaliza kidato cha nne na cha sita na ni wangapi wanakwenda chuo kikuu.

Ni wangapi wamemaliza vyuo vikuu na kuingia TRA, Benk kuu na mashirika ya kimataifa.

Wanamitandao ya kuwaunganisha wote bila kujadili itikadi ya vyama vya siasa wala makundi ya wanasiasa.

Sio kama hapa Nzega, ukiwa hauko katika kundi la Bashe basi wewe ni mbaya na ni adui wake na kundi lake, watakufanyia kila hila, fitina, ubaguzi na hata kukutengenezea kesi za kila aina. Nayasema haya kwa sababu nayajua, wengi wa watu wameumizwa na kundi hili na mimi nikiwemo, kuna mpaka watumishi wa umma wapepata misukosuko ya kushangaza na hata wengine kuhamishwa kabisa.

Sasa hivi watymishi wengi wameufyata, wamekuwa romoti anawapelekesha vibaya, tena wakati mwingine kupitia wapembe wake tu.


Hivyo, mikoa ambayo watu wake wanajitambua hawana siasa za chuki, wala hawajadili wali na nyama kama ilivyo huku, bali wanajadili maendeleo ya elimu ya watoto wao. 

Kuna mikoa inajulikana kwamba suala la kilimo na ufugaji halina itikadi za vyama vya siasa; mpango ni kutafuta soko la kuuza mifugo na mazao. Kutafuta masoko ya mazao.

Watu hawa hawana muda wa kujadili wali na nyama, bali ni kutaka kujua mbunge au kiongozi wao ana mpango gani wa kuwatafutia soko la kuuza mifungo au mazao yao.

Watu kama hawa huwezi kuwashawishi kuja mkutanoni kwa kuwapikia wali na nyama, wala kwa elfu kumi au 30 nk, bali unaweza kuwashawishi kwa kuwatangazia bei ya juu ya mazao yao na bei ya juu ya mifugo yao.

Na kama kuna mtu anataka kugombea na kupiku ubunge wa maeneo haya atajitahidi kucheza na bei ya mifugo na mazao na wala si kupika wali na nyama.

Nafikiri msomaji utakuwa umeielewa hoja yangu hapa na ninachomaanisha, kwamba hoja yangu hapa wala si kupinga watu wasipikiwe wali na nyama, bali nataka ieleweke kimantiki kwamba, wabunge ni wawakilishi wa wananchi, na katika hali ya kawaida ni lazima waishi kwenye jamii wanayoiwakilisha.

Hivyo mbunge kuandaa chakula na kula na wananchi anaowawakilisha si jambo la kushangaza.

Wakati wakila, wanaweza kujadili mambo mengi juu ya maisha yao ya kila siku. Wakati wa mazungumzo, wakiacha kujadili maendeleo, wakaanza kumsifia mbunge wao kwa kuwapikia wali na nyama na kuwpatia pombe, akitokea mwandishi wa habari ambaye hilo limemkera, akaandika, inaweza kueleweka.

Lakini kama watu wamekula wali, nyama na kunywa pombe na baadaye wakaanza kujadili mambo ya maendeleo, na mwandishi wa habari, akaacha kuandika juu ya mambo ya maendeleo yaliyojadiliwa, akaandika juu ya wali na nyama ni kuonesha hitilafu kubwa katika kufikiri na kuchambua masuala ya kisiasa.

Hivyo, ni wazi kwamba mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini, Dk. Hamis Kigwangalla, kuna mambo amefanya na mengine hajafanya, katika uchaguzi mkuu mwaka huu ushindani wa kweli ni kumpongeza kwa mazuri aliyofanya na kumbana kwa yale aliyoshindwa kuyafanya.

Huu ndiyo itakuwa uungwana, na kwa mtu ambaye ni makini anahitaji kuongoza wananchi wa jimbo hili, na anapenda maendeleo ya wilaya yetu ya Nzega, itakuwa vizuri muda ukifika aanze na kwa kututajia mahitaji ya jimbo au wilaya yetu kwa ujumla, kiasi ambacho mbunge husika amechangia na ni kiasi gani bado.

Na kueleza mikakati yake ya kutekeleza yale ambayo ni bado, huyo ndiyo tutasema ni mwanasiasa mwenye maono na si mbabaishaji.

Huu unaweza kuwa ushawishi kwa upande wa ye yote yule anayetaka kuingia kwenye uwanja huu wa siasa; akijua ni yapi ya kutekeleza ili kufanya uwakilishi kikamilifu.

Mtu anayekuja kwa sababu amesikia kuwa mbunge aliyepo "Dk. Kigwangalla hapokeagi simu" sidhani kama atakuwa ana vision ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Nzega Vijijini, wala kusema ana nia njema na Wilaya yetu kimaendeleo.

Sisi tumezunguka karibu wilaya nzima likiwemo jimbo hili na kuona namna lilivyo kubwa, ubora wake na changamoto zake, baadhi ya ubora na changamoto tumezieleza kwenye makala ya kwanza ya jimbo la Bukene na tulifanya hivyo kwa sababu kijiografia yanafanana kwenye ardhi na mazao hasa yale ya kimkakati(kibiashara) yanayolimwa na yale yanayoweza kulimwa.

Shida kubwa katika majimbo haya kiuchumi ni kwamba wanasiasa hawaji na suluhisho la uwekezaji kwenye mazao ya kimkakati au yale ya kibiashara.

Madhaifu na ubora wa Dk. Kigwangalla kiuongozi ni yapi? Hayo tukutane makala ya mwisho ijayo..

Kwiyeya Singu 0784977072



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI