Bakari George Makamu Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru.
Na,Jusline Marco;Arusha
Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru iliyopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe. Japhet Hasunga akizungumza katika ziara hiyo amesema kamati imeridhishwa na ujenzi wa jengo hilo ambao umekidhi ubora unaokidhi vigezo na matumizi sahihi ya fedha.
Aidha amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii kuwasiliana na Wizara ya fedha ili kufanikisha upatikanaji wa fedha za kumalizia ujenzi wa jengo hilo.
Kwa upande wake Bakari George Makamu Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru akitoa taarifa mbele ya Kamati hiyo amesema Mradi huo ulianza Mei 17 mwaka jana na unatarajiwa kukamilika Mei 17 mwaka huu ambapo amesema utaratibu unaotumika katika utrkelezaji wa ujenzi huo ni utaratibu wa mkandarasi mzawa.
Aidha amesema jumla ya gharama za ujenzi katika mradi huo ni shilingi Bilioni 5.6 ambapo mpaka sasa kiasi ambacho kimepokelewa ni shilingi bilioni 2.7 ikiwa ni asilimia 47.7 ya fedha zote za utekelezaji wa mradi huku mfadhili mkuu wa mradi akiwa Serikali kuu ambapo amesema jengo hilo litakapokamilia litakuwa na ofisi 44 zenye uwezo wa kuhudumia watumishi 94,litakuwa kumbi 5 za mikutano zenye Uwezo wa kuhudumia watu 545.
Ameongeza kuwa mpaka sasa mradi huo umefikia 70 ya utekelezaji wake ambapo katika muda uliotumika wapo nyuma ya utekelezaji kwa asilimia 5 na wapo mbele kwa utekelezaji kwa asilimia 22.3 kwa kuzingatia kiasi cha fedha ambazo zimepokelewa huku akieleza kuwa uwepo wa mradi huo wa kimkakati kutawezesha kuchochea na kuongeza tija mahali pa kazi.
Dkt.Bakari ameeleza kuwa kuongezeka kwa nguvu kazi kunatakiwa kuende sambamba na upatikanaji wa ofisi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yao ambapo amesema kiasi ambacho kinatarajiwa kukamilisha ujenzi wa mradi huo ni shilingi bilioni 2.9 na kufanya jengo hilo kukamilika kwa asilimia 100.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Amir Mkalipa kama msimaizi wa serikali ya Wilaya amesema atahakikisha maelekezo yaliyotolewa na kamati hiyo na ushauri unafanyiwa kazi ambapo pia amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kutoa fedha hizo ili kuweza kupunguza changamoto za ofisi katika chuo hicho.
Mwisho.
0 Comments