Header Ads Widget

COMNET ZANZIBAR MABINGWA WA RESI ZA NGALAWA ZIFF2026


Na. Mwandishi Wetu, Zanzibar.


KAMPUNI ya kutoa Huduma za Internet ya Comnet, wameibuka mabingwa wapya wa resi za Ngalawa zilizofanyika ufukwe wa Serena, Unguja Alasiri ya leo Juni 28, 2026 katika  kuhitimisha Tamasha la 29 la Kimataifa la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) kwa mwaka huu.

Katika resi hizo, Ngalawa 11ziliweza kushiriki na Comnet kuibuka washindi baada ya kuwashinda washiriki wengine 10.

Mtendaji Mkuu wa ZIFF, Joseph Mwale, amewatangaza washindi hao mbali na na Comnet kuongoza, wengine ni:

Mshindi wa Pili kampuni ya Azam Media, mshindi wa tatu ZIFF, na mshindi wa Nne ni Robin Batista.




Washindi wengine ni: Zanzibar Marine Association (Z.M.A), Fish market, ZIFF, WIOMSA, UN Women, na wengine.

Katika tukio, hilo Mjumbe wa Bodi wa ZIFF, Prof. Martin Mhando aliweza kutoa neno na zawadi kwa washindi hao washiriki.

Kihistoria na kitamaduni, mbio za ngalawa zimekuwa kielelezo kikuu cha maisha, ukakamavu na urithi wa Waswahili wa mwambao ambao wametumia vyombo hivi kwa karne nyingi katika uvuvi na usafiri. 

Kuingizwa kwa mashindano haya kama kilele cha tamasha kupitia jukwaa la Wanawake na Vijijini (Women Panorama) kunalenga kuhuisha mchezo huu wa asili na kuupa sura ya kisasa inayovutia watalii na wenyeji. 

Tukio hili la kasi na ufundi majini halimalizi tu tamasha kwa burudani, bali linaweka msisitizo mkubwa katika agenda ya mashindano yenyewe kama nguzo inayounganisha jamii, huku ufukwe wa Serena ukigeuka kuwa uwanja wa mayowe, shangwe na ushindani wa kweli wa baharini.
























Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI