Na Lilian Kasenene,Morogoro
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC) Jaji wa mahakama ya Rufani Jacob Mwambegele amewataka watendaji mkoa wa Morogoro kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao na kukabiliana na changaamo zitakazojitokea wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Aidha Jaji Mwambegele akawataka watendaji hao kufanyakazi yao kwa weledi, bidii,moyo wa kujituma na maarifa.
Alisema hayo wakati wa mafunzo kwa watendaji wa ngazi ya Mkoa kuhusu uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura mkioa wa Morogoro, yenye kauli mbiu ‘Kujiandikisha kuwa Mpiga kura ni msingi wa uchaguzi’.
Jaji Mwambegele alisema wakati wa uboreshaji wa daftari ni matarajio ya tume kuwa kila mmoja kwa kutumia ujuzi, uwezo na uelewa wao kwa kusimamia na kuendesha zoezi hilo la uboreshji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa umakini ili kutekeleza majukumu ya kitaifa.
“Naimani kila mmoja atapata elimu na ujuzi wa kutosha utakao mwezesha kutekeleza majukumu ya kitaifa ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2025,”alisema.
Akaeleza kuwa, maafisa Teknolojia Ya habari na Mawasiliano (TEHAMA) watapatiwa mafunzo maalumu ya jinsi ya kukabiliana na chambamoto mbalimbali za kiufundi endapo zitajitokeza wakati wa zoezi hilo la uandikishaji wa daftari hilo la wapiga kura.
Akawasii wale waliowahi kushiriki katika majukumu ya tume kwa kuratibu na kusimamia katika awamu zilizopita kwa kuwasaidia ambao hawakuwahi kushiriki ili waweze kufanikisha zoezi hilo ili waweze kupata uelewa wa pamoja.
Mweyekiti huyo akataja asasi zilizopatiwa kibali ambapo alitaja kuwa asasi 157 za kiraiya kwa ajili ya kutoa elimu ya mpigakura, ikatoa kibali kwa taasisi na asasi za kiraiya 42 kuwa wangalizi watakao shiriki katika zoezi la uboreshaji wa daftrari la kudumu la mpiga kura kati ya hizo taasisi tisa za kimataifa na taasisi 33 ni za ndani ya nchi.
Mmoja wa washiriki afisa mwandikishaji jimbo la Morogoro mjini Faraja Maduhu alisema hiyo ni hatua muhimu kuelekea zoezi hilo la uandikishaji kwa wataalamu wa kisekta na kwamba wamekula kiapo na watasimamia kikamilifu yale yote waliofundishwa na kuyatekeleza.
Maduhu akawataka wananchi kutoka makundi mbalimbali kujitokeza wakati wa zoezi hilo la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Mwisho
0 Comments