Header Ads Widget

SULUHU YA MIMEA VAMIZI NDANI YA BONDE LA KRETA NGORONGORO YAANZA KUTAFUTIWA UFUMBUZI.

 

Na,Jusline Marco;Ngorongoro.

Ujumbe wa wataalam kutoka Jamhuri ya Cuba wakiambatana watalaam wa uhifadhi kutoka Wizara ya Maliasilii na Utalii wametembelea bonde la kreta lililopo Eneo la Hifadhi ya  Ngorongoro kwa ajili ya kuona hali halisi ya uwepo wa mimea vamizi ndani ya Bonde hilo. 


Akizunguza wakati wa ziara hiyo  Dkt. John Bukombe  Kutoka taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) amesema lengo la ziara hiyo ni hatua za awali za kutafuta namna ya kukabiliana na changamoto ya mimea vamizi kwenye maeneo yaliyohifadhiwa. 

Amesema watasaidiana na wataam hao kutafuta namna ya kukabiliana na changamoto ya mimea vamizi inayoathiri uoto wa asili ndani ya bonde la  Kreta ambayo kwa kiasi kubwa imesababisha kutoweka kwa  mimea asili ambayo ni malisho ya wanyamapori.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Kitengo cha Usimamizi wa Wanyamapori na Utafiti, Afisa Uhifadhi Mkuu Lohi Zakaria amesema kuwa  NCAA imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kudhibiti mimea vamizi ndani eneo la Hifadhi, jitihada ambazo bado hazijazaa matunda yaliyotarajiwa.


Dkt. Orlando Enrique Sanchez Leon ambaye ni mkuu wa ujumbe wa wataalam kutoka Cuba ameeleza kuwa wameona tatizo la kuwepo kwa mimea vamizi ndani ya bonde la kreta ambapo pamoja na sababu zingine mwingiliano wa shughuli za binadamu na Wanyamapori unaweza kuwa chanzo cha uwepo wa mimea hiyo hifadhi hapo.


 Amesisitiza kuwa wapo tayari kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wataalam wake kuhakikisha kuwa kutapatikana mbinu bora za kuthibiti mimea hiyo vamizi ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI