Header Ads Widget

WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYA YA CHAMWINO WASHEHEREKEA KUMBUKIZI YA MIAKA 48 TANGU KUANZISHWA KWA CHAMA HICHO



WAKATI chama cha Mapinduzi CCM kikiwa kinafikisha miaka 48 tangu kuanzishwa kwake viongozi wa chama hicho pamoja na viongozi wa serikali wametakiwa kujitathimini kuhusu utekelezaji wa malengo yao ndani yachama

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi na MNEC, Donald Megitii, amesema hayo Leo jijini hapa wakati wa ufunguzi wa Sherehe za miaka 48 tangu kuanzishwa kwake ufunguzi uliofanyika Wilayani Chamwino  Kata ya Ikoa kijiji cha Makoja. 

MNEC huyo amesema Sherehe hizi za kihistoria zinatoa fursa muhimu kwa viongozi kukumbuka ahadi zao za kusimamia haki na ustawi wa jamii humuhimu wa kuimarisha haki na amani, akitahadharisha kwamba ni jukumu la viongozi kufanya kazi kwa karibu na wananchi ili kuhakikisha haki za kila mtu zinaheshimiwa

Megitii ameeleza kuwa CCM ni nguzo muhimu katika kuondoa dhuruma na unyanyasaji, huku akihimiza kuwa huduma za kijamii zinapaswa kuwafikia wananchi wote.

"Hii ni fursa ya kutathimini mafanikio na changamoto, huku mwaka huu ukiwa wa uchaguzi wa madiwani, wabunge, na Rais, "

Na kuongeza"Hivyo CCM inatarajia kushinda kwa kishindo, ikikumbuka lengo lake la msingi la kuwatumikia wananchi," amesema Megitii.

Katika ujumbe wa matumaini, Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga, aliwaomba wananchi wa wilaya ya Chamwino kuhakikisha chama kinashinda tena kwa nguvu katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025. 

"Kama tulivyofanya vizuri kwenye uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa, ambapo tulishinda kwa asilimia 100 katika kata, vijiji, na vitongoji, basi tukafanye hivyo pia katika uchaguzi wa Rais, wabunge, na madiwani," alisema Mbaga.

Kilele cha maadhimisho haya kinatarajiwa kufanyika tarehe 5 Februari katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo viongozi na wanachama wa CCM watakusanyika kuadhimisha mafanikio na kuelekeza mikakati ya baadaye.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI