Header Ads Widget

TANZANIA KUWAFIKIA WANANCHI MILIONI 8.3 NISHATI YA UMEME KUFIKIA 2030.


NA NAMNYAKI KIVUYO,ARUSHA

Tanzania imejipanga kuwapatia wananchi milioni 8.3 nishati ya umeme ifikapo mwaka 2030 ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha  wawekezaji binafsi kuwekeza katika uzalishaji wa umeme katika visiwa vilivyopo ziwa Victoria pamoja na Mafia.

Hayo yamesemwa na Naibu mkurugenzi mtendaji anayeshughulika na uzalishaji wa  shirika la umeme Tanzania(TANESCO) Mhandisi Costa Rubagumya katika mkutano wa ushirikiano wa sekta za nishati Afrika Mashariki ambapo alieleza kuwa wapo katika mkutano huo wapo kuangalia watakavyoshirikiana kufikia malengo hayo mojawapo ikiwa ni kuwafikia wananqchi kuwanzia uzalishaji, usafirishaji, usambazaji.

"Tunataka kuwafikia hata wale ambao gridi zetu za taifa haziwezi kufika huko kwa maana ya kuwa na Mini-grids ambazo zitawafikia hasa katika Visiwa vilivyopo ziwa Victoria na kisiwa cha Mafia bahari ya Hindi ambapo ndipo tunapovutia wawekezaji kufika na kuwekeza kwenye umeme kwa bei ambayo wananchi wa kule wataweza kumudu,"Alisema Mhandisi Rubagumya.

"Serikali imeweka mazingira mazuri katika uwekezaji wa umeme wa jua pamoja na umeme wa upepo lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wawekezaji  watakapowekeza umeme utakaopatikana utakuwa ni wa bei ambayo wananchi wananchi wanaweza wakahili,"Alieleza

Alifafanua kuwa wameeleza vivutuo vilivyopo Tanzania kwaajili ya wawekezaji kwaajili ya kuhakikisha lengo la kuwafikia wananchi linakamilika  ambapo TANESCO  wamekuwa wakiwaonga wateja 500,000 kila mwaka  lakini kwa malengo haya mapya kwa mwaka wanatakiwa kuwafikia wateja 1,600,000.

" Ukiangalia ni mara tatu  ya tulivyokuwa tunafanya, ndio maana tunawaita wawekezaji kwasababu  TANESCO  haiwezi peke yake tunachohakikisha ni mazingira yanakuwa mazuri kwa wao kuwekeza ili kulifikia hilo lengo,,"Alifafanua.

Kwa upande wake Dkt Joseph Siror mkurugenzi wa kampuni ya Kenya Power and lightning (KPLC) alisema kuwa wakiungana pamoja kama Afrika Mashariki wanaweza kuhakikisha kuwa nishati wanayotumia watu iwe ya bei nafuu kwa kuangalia mahitaji ya Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda, Burundi mpaka DRC Congo.

"Bei ya nishati inategemea ni teknolojia gani umetumia kuzalisha hiyo nishati ambapo badaya ya kutumia ya bei ya juu ambayo inalazimika pale umeme umapokuwa hautoshelezi basi tushirikiane badala ya kwenda kwenye ghali unaweza kumia wa nchi ya jirani ambayo ni ya bei ya chini,"Alieleza Dkt Siror.

Naye mkurugenzi wa uzalishaji wa jumuiya ya Afrika mashariki Jean-Baptiste Havugimama  alisema kuwa katika nchi wanachama wanahitaji kujenga mazingira mazuri ambayo muwekezaji ataweza kuwa na nguvu na uwezo wa ununuzi ili mtumiaji aweze kumudu gharama za umeme.

"Tunapaswa kuhakikisha nishati zinazotengenezwa zinatumiwa na nchi zingine hii iitasaifia kutokupotea kwa nishati lakini pia kupunguza bei na kuwa na bei ambayo mwananchi wa mwisho kabisa  anaweza kulipia,"Alieleza.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI