Lilian Kasenene,Morogoro
Matukio DaimaApp
MKURUGENZI Bodi ya Bonde Wami Ruvu Elibariki Mmasy amesema wamezindua mfumo wa utabiri wa hali ya maji katika vyanzo vya maji ili kubaini kiwango cha maji na kutoa taarifa.
Amesema hayo mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.
Amesema kupitia mfumo huo wanaunganisha taarifa hizo kwa mamlaka ya hali ya hewa na kwamba unapima mtiririko wa maji ambao unaonyesha kiwango cha maji na hata kubaini kama kunaviashiria vya mafuriko .
"Bodi ya bonde kwa sasa tumetengeneza mfumo ambao unapima mtirirlo wa maji na kutabili maji yaliyopo kwenye mbalimbali vya maji na kutabili huo itakuwa unatolewa Kila baada ya siku kumi kujua Hali ya Maji,"alisema.
"Mto Ruvu wote tunasimamia na Hali kadhalika maeneo ya vyanzo vina majinya kutosha chini na juu ya Ardhi na mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Pwani na Morogoro, maji yanakidhi na Kila Alhamisi tutaendelea kutoa taarifa zetu na tunaungana na TMA,"alisema.
Hata hivyo amesema kwa sasa vyanzo vyote vya maji vina maji ya kutosha kwa matumizi ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Dodoma na Morogoro ambao wanategemea maji kutoka mto Ruvu.
Aidha amesema bado kumekuwa na changamoto ya wakulima na wafugaji pamoja na wachimbaji wa mchanga bila kuwa na vibali ambapo wameendelea kutoa elimu kwa wale wote wanaofanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo hayo.
"Kama taasisi tumeendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji lakini bado watu wanaendelea kufanya hizo shughuli,naomba wananchi waheshimu mita 60 zilizopo kisheria na tunachosimamia sisi ni kwa manufaa na kustakabali wa taifa letu," alisema.
Awali msimamizi wa kidakio Cha Ruvu Paschal Joseph akiwasilisha kwa wanahabari namna bodi unavyofanya kazi kwenye maeneo yake, amesema kama taasisi wameweza kurejesha kilometa 16.1 ya mito iliyopoteza uelekeo wake kutokana na sababu mbalimbali ikiwwmo shughuli za kibinadamu zinazofanywa na wananchi.
Akashauri Wizara ya Kilimo, mifugo na wananchi kwa ujumla kuchimba mabwawa ya kuhifafhi maji wakati huu wa mvua za masika ili yaweze kusaidia wakati wa kiangazi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya amesema ushirikiano uwe wa mwendelezo na kwamba wanahabari watafanya kazi kwa nia ya kuwafikisha wananchi taarifa juu ya uwepo wa Bodi ya bonde la Wami Ruvu.
"Sisi kama wanahabari milango Iko Wazi na kwamba wanahabari Wana wajibu wa kuhakikisha wanafanyakaxi ya kuhabarisha wananchi.
0 Comments