Header Ads Widget

DC MOROGORO AWAASA WAZAZI KUTOWAFICHA WATOTO WENYE ULEMAVU

MKUU wa wilaya ya Morogoro Bw Mussa Kilakala amewaasa wazazi na Walezi kutowaficha watoto wenye ulemavu badala yake wahakikishe wanapatiwa huduma za msingi ikiwemo kupelekwa shule kwani Serikali ya awamu ya sita imewekeza kwenye elimu ili kila mtoto aweze kupata elimu stahiki. 

Mkuu huyo wa Wilaya alisema hayo mjini Morogoro katika wakati akikabidhi msaada wa vitimwendo 30 vya thamani ya shilingi milioni 10.5 vilivyotolewa kupitia yeye na msamaria mwema mmoja kutoka jijini Dar es salaam.

Kilakala akasisitiza jamii kuacha kuwaona watoto wenye ulemavu kuwa ni laana badala yake wawatoe na kuwapa huduma zote za msingi kwani wakiwezeshwa wanaweza.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Morogoro Bi Ruth John aliwaasa wazazi nao na walezi kukubaliana na hali ya ulemavu wa watoto wao kwani ni mapenzi ya Mungu na wasiwafiche badala yake wawatoe wapate huduma.

Aidha baadhi ya watu wenye ulemavu waliofaidika na msaada huo Seleiman Habibu, Juliana Kimungu anayemlea mjukuu wake mwenye umri wa Miaka kumi na moja Careen George na Rehema Senga ambaye ni mama Lishe walishukuru kwa msaada huo ambao sasa utawawezesha kusogea kutoka eneo Moja kwenda jingine wakati wowote bila shida ikiwemo wakati wa mvua ambapo hali huwa ni ngumu zaidi.

Rehema akasema katika shughuli zake za biashara ya mama lishe alikuwa akisogea kwa kusota na makalio lakini kitu alichopata kitamrahisishia na kuondokana na utegemezi 

Wakashauri Serikali kuwapatia mikopo ilj kujikwamua kiuchumi kupitia asilimia kumi za kwenye halmashauri ambapo manispaa ya Morogoro imetenga shilingi bilioni moja na milioni 300 kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu.





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI