Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI WA MAJI AKIRI KUTORIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI LUNYANYWI NJOMBE

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Naibu waziri wa Maji Kundo Mathew amekiri kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa kutibu maji unaojengwa kwa ufadhili wa serikali ya India huko Lunyanywi Mkoani Njombe huku akiagiza kuongezwa kwa nguvu kazi.

Akikagua mradi huo hii leo,Naibu waziri Kundo amesema Mradi huo upo nyuma ya utekelezaji kwa miezi mitatu hivyo mkandarasi anapaswa kuongeza wafanyakazi watakaofanyakazi usiku na mchana.

Awali Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Njombe mjini Mhandisi Robert Lupoja Amesema Mradi huo unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 40 na utatekelezwa kwa miezi 26.

Mhandisi Lupoja amesema endapo mradi huo utakamilika na kusambazaji maji kwa wakazi wa mji wa Njombe utahudumia zaidi ya watu elfu 99 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Yusta Falo na Alexender Fute ni wakazi wa Njombe ambao licha ya kushukuru kwa kutekelezwa kwa mradi huo lakini wanaiomba serikali iharakishe kuutekeleza kwani adha ya kupata maji ni kubwa kwao hususani kwa wanaoishi mtaa wa Msete.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI