Header Ads Widget

AZAM MASHUJAA MECHI YA KISASI LAKE TANGANYIKA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

Kocha wa timu ya soka ya Azama Rachid Taoussi amesema kuwa muda mfupi tangu kumaliza mechi na Simba na umbali mrefu kutoka Zanzibar hadi Kigoma umemnyima nafasi nzuri ya mapumziko kwa wachezaji wake kujiandaa kikamilifu dhidi ya mchezo wao na timu ya Mashujaa unaotarajia kufanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma Jumapili Septemba 29/

 

Kocha huyo raia wa Morocco alisema hayo mkoani Kigoma kuelekea mchezo huo na Mashujaa alibainisha kuwa wachezaji wake walitumia nguvu kubwa kwenye mchezo na Simba hivyo walihitaji kupumzika kabla ya kusafiri umbali mrefu kuikabilia mashujaa.

 


Pamoja na hilo kocha huyo alisema kuwa hawatakubali kupoteza tena mechi na Mashujaa baada ya kudondosha pointi tatu kwa Simba kwenye mchezo uliopita na kwamba wamefika Kigoma wakiwa timamu kupambana kuhakikisha wanapata ushindi na kwani  kila mechi kwao wanaichukulia kwa uzito mkubwa kuelekea kwenye mbio za ubingwa.

 

 

Akizungumzia mchezo huo Kocha wa timu ya mashujaa Mohamed Barres ambaye timu yake  inatarajia kushuka dimbani Septemba 29 kumenyana na timu ya Azam FC amesema kuwa wanaiheshimu timu hiyo kwa ukubwa wake na aina ya wachezaji iliyo nayo lakini ameonya kwamba Azam haitatoka na ushindi kwenye mchezo wao wa jumapili.

 


Kocha huyo wa Mashujaa alisema kuwa wanajua Azam ina kiu ya ushindi baada ya kupoteza mchezo wake na Simba lakini hilo haliwatishi na kwamba vijana wake wako tayari kukabili mchezo huo na kupata ushindi kwani wamejipanga vizuri kuondokana na ushindi kwenye mchezo huo.

 


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI