Header Ads Widget

VIJANA 1000 KUNUFAIKA MRADI WA KONGANI YA VIJANA KAGERA.

 


Na Mariam Kagenda _Kagera 


Mwenge wa Uhuru Umeweka Jiwe la Msingi na Kuzindua Mradi Wa Kongani ya Vijana Ambao Umeghalimu Zaidi Ya Shilingi Milioni Kumi na Saba Ambao Utawanufaisha Vijana wanaofanya Shughuli za Useremala,Uchomeleaji Pamoja Na Shughuli za Ufundi wa Vijana.


Mradi Wa Kongani ya Vijana Uliopo Kata Ya Bilele Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera ni Mradi Wa Sera ya Uwezeshaji wa Vijana Kwa Mwaka 2007 Iliyohusishwa Mwaka 2024 na Utekelezaji wa Mpango wa Mwaka  2024 Mpaka 2034 na Mradi Huu Unategemea Kuwanufaisha Vijana Zaidi Ya Elfu Moja Katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.



"Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2024, Katika kutekeleza sera ya vijana ya mwaka 2007 iliyohuishwa 2024 na utekelezaji wa mpango wa mwaka 2024- 2034, tumeanzisha Kongani ya vijana wanaofanya shughuli za Useremala, Uchomeleaji, Ujasiliamali mdogo, Uoshaji wa magari na baadae tunakusudia kuanzisha SACCOs ya Vijana. Kituo hiki kinaanza na vikundi 2 vya vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi kutoka vyuo vya ufundi stadi (VETA), vikundi 2 vya vijana vilivyonufaika na mkopo wa 4%, kikundi kimoja cha Abagambakamo (wajasiriamali) na kikundi cha Nakihahe"Amesema Rwiza Venant



Mradi Huu Utawawezesha vijana kujiajiri kwa ajili ya kuinua uchumi wao kwa kuwaunganisha pamoja na kuwa na eneo moja kwa ajili ya kufanyia shughuli za kujiingizia kipato, Kuwawezesha vijana kukuza ujuzi na kutoa ajira kwa vijana wengine ili kupunguza utegemezi kwa vijana Na Kuondoa Umasikini Kwa Vijana. 


Mwenge Wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2024 Umeenda Na Ujumbe Usemao "TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI