Header Ads Widget

CCM MORO YASEMA HAKUNA KUBEBA WAGOMBEA MIZIGO KWENYE UCHAGUZI

 


Na Ashton Balaigwa,MOROGORO

MJUMBE wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa (Mnec) kupitia Mkoa wa Morogoro,Jonas Nkya,amesema wagombea 
mizigo wanaokigharimu chama hicho na wasiokubalika  kwa wananchi mwisho wao umefika na kuwataka  viongozi wa Chama hicho, kuacha upendeleo wa  kuwabeba wakati wa kipindi hiki cha kuelekea kwenye chaguzi mbalimbali ukiwemo wa Serikali za Mitaa.  

Badala yake  amesema viongozi hao wa CCM  watoe  haki na  kutumia busara katika mchakato wa kumpata mgombea anayekubalika kwa wananchi ili  chama hicho kipate  ushindi mkubwa wa kuendelea kushika madaraka ya uongozi.

Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu wa CCM,alisema hayo mbele ya Waandishi wa Habari  wakati akipongeza jitihada za Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa vyombo vya usafiri wa Pikipiki kwa viongozi wa kila kata wa chama hicho Mkoani Morogoro.

“ Viongozi wenzangu wa CCM Mkoa wa Morogoro,tuache hii tabia ya kubeba wagombea ambao ni mizigo,wakati huo kwa sasa umeshapitwa na wakati kwani tutakighalimu chama,tuwapitishe wagombea wanaokubalika na kupendwa na wananchi ili tupate ushindi kwenye chaguzi zinazokuja” alisema Mnec huyo.

Nkya alisema tayari Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Rais Samia Suluhu Hassan,ameshaonyesha njia kwa viongozi kupitia chama hicho ni lazima wafanye kazi na kutatua kero za wananchi na wasitegemee kuja kubebwa kwenye chaguzi zinazokuja huko mbele.

Hata hivyo Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya CCM ,alikumbusha viongozi hao kuwa sifa kuu ya mkoa wa Morogoro ni mkoa wa chama hicho ambao kila chaguzi umekuwa ukitoa kura nyingi kwa wagombea wa nafasi mbalimbali  ikiwemo zile za Urais.

“ Mkoa wa Morogoro una sifa ya kuitwa mkoa wa CCM kwasababu kila chaguzi wagombea kupitia chama hicho wamekuwa wakishinda kwa  kura nyingi sana kwenye chaguzi mbalimbali ikiwemo Urais,Ubunge na Udiwani sasa tuna kila sababu ya kulinda kula hizo kwa kuweka wagombea wanaokubalika” alisema Mnec Nkya.

Hata hivyo,aliwataka kundi la vijana kupitia chama hicho kujitokeza kwenye misingi ya kisiasa ya Ujasili,Uthubutu na  kutokubali kukata tamaa ili kugombea nafasi mbalimbali katika chaguzi ukiwemo wa mwaka huu wa Serikali za mitaa ili kukiwekea mazingira mazuri chama hicho.

Nkya ambaye pia  Mwenyekiti  mstaafu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) alisema vijana hao wa kila sababu ya kugombea nafasi hizo na kuibuka washindi kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ya utekelezaji wa ilani ya CCM kupitia miradi mikubwa ya kimakati kwenye sekta mbalimbali.

Naye  Diwani kijana  wa Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro,Samuel Msuya(CCM)alihamasisha kundi la vijana kuacha hofu ya kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakidhani zipo kwaajili ya Wazee na waliostaafu tu dhana ambayo alisema ni potofu.

“ Tuacha uoga vijana,tujitokeze kugombea nafasi mbalimbali kwenye chaguzi kupitia CCM ,kamwe tusikubali maneno ya kukatishwa tamaa eti nafasi za uongozi zipo kwaajili ya wazee tu angalieni wenzetu wa vyama vingine mbona vijana ndio wanajitokeza kuwania nafasi za uongozi,

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI