Header Ads Widget

WANAWAKE MORO WAAMKA KWA KISHINDO KUCHUKUA FOMU ZA UDIWANI

 


Asilimia 70 ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Morogoro waliorejesha fomu za kuwania nafasi za udiwani ni wanaume, huku wanawake wakichangia asilimia 30 ya waombaji wote, hali inayotajwa kuwa ya kipekee katika mkoa huo ambao umeendelea kuwa na mwitikio mkubwa kisiasa.


Takwimu zilizotolewa na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Morogoro, Zangina Shanang Zangina, zinaonesha kuwa kati ya wanachama 1,384 waliochukua fomu, 1,381 walizirejesha. Kati ya hao, wanaume ni 1,177 na wanawake ni 204 kwa upande wa nafasi za kata katika kata zote 214 za mkoa huo.


Kwa upande wa viti maalum kupitia Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), jumla ya wanawake 297 walichukua fomu, ambapo 290 walizirejesha ndani ya muda uliopangwa. Hali hiyo inafanya jumla ya waombaji kufikia 1,681, hatua inayotajwa kama sehemu ya maandalizi makini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.


Zangina amesema kuwa hatua inayofuata baada ya urejeshaji wa fomu ni vikao vya mchujo vilivyoanza Leo  ngazi ya kata, ambapo majina matatu ya kila nafasi yatawasilishwa kwa kura za maoni na baadaye kupelekwa kwenye mikutano mikuu kwa ajili ya uteuzi


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI