Header Ads Widget

WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MITWERO WAIPIGA JEKI SHULE MADAWATI


NA MATUKIO DAIMA MEDIA, LINDI 

 Wanafunzi walio hitimu  darasa la 7 mwaka 2002 shule ya msingi Mitwero iliyopo kata ya Rasibula  manispaa ya Lindi wametoa msaada wa madawati 8 yenye thamani ya Sh 780,000 katika shuleni hiyo.


Zoezi hilo la kukabidhi  madawati hayo lime fanyika leo tarehe 04,07,2025 shuleni hapo na kupokelewa na mkuu wa wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva. 


Wakati wakikabidhi madawati hayo wahitimu hao wamesema wako tayari kuendelea kushirikiana na serikali katika kuendelea kufanya ukarabati katika shule hiyo na wapo tayari kuchangia kwenye ukarabati wa madarasa yalio chakavu.


Mosses Verisi  mwenyekiti wa umoja wawahitimu hao akizungumza kwa niaba ya wenzake amesema wako tayari kuchangia maendeleo ya shule hiyo na Mungu akipenda mwakani watakuja na kitu kingine cha kuchangia.



" kwa umoja wetu tuliamua tujikusanye tuje tutembelee shule yetu tukaona kuna uchakavu wa majengo lakini kwakuanzia leo tumekuja na madawati 8  nikidogo lakini naamini kitasaidia kwakuokoa wanafunzi wachache kukaa chini.Leo sio mwisho kwa umoja wetu tutaendelea kuchanga na Mungu akipenda mwakani tutakuja na kitu kingine"amesema Mosses Mwenyekiti wa wanafunzi walio soma shuleni hapo.


Mwenyekiti huyo wa umoja wa wanafunzi hao ameendelea kwakusema wapo tayari kuaendelea kuchangia na utakapo anza ukarabati wa  majengo wapewe taarifa ili waweze kushiriki.


"Haijalishi mtu anaishi wapi wengine tunaishi nje ya Mitwero lakini tumeshirikiana tumeleta hiki kidogo Tunauwomba uongozi wa elimu itakapotokea kunaukarabati wa madarasa mtujulishe ili na sisi tuweze kuchangia kwa kile kidogo tutakacho kipata"amesema Mosses mwenyekiti wa umoja wa wanafunzi hao walio soma shuleni hapo.


Kwaupande wake makamo mkuu wa shule  ya msingi Mitwero    Amina Mohamedi amesema shule yao ilikuwa na uhaba wa madawati 45 kwakuyapata hayo madawati 8 yamewasogeza kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.



"Tulikuwa na upungufu wa madawati 45 leo tumeyapokea madawati haya 8 tunashukuru sana kwasasa tumebakiwa na upungufu wa madawati 37 niwaombe na wengine walio soma hapa waje watuunge mkono kwa changamoto zingine tuna nadarasa chakavu yana vuja kwahiyo tunawakaribisha waje watusaidie"amesema Amina makamo mkuu wa shule ya msingi Mitwero.


Baadhi ya wanafunzi wa darasa la Saba  shule ya msingi Mitwero Yasini Stiven na  Agnes Raymond wameshukuru kwa msaada wa madawati walio patiwa na kuahidi kufanya vizuri katika mitihani yao.


"Madawati haya yatatusaidia kuondoa kero ya kubanana wakati wakukaa darasani na kwa wale wanafunzi watoro watafika shuleni kwasababu madawati yapo na watapata sehemu za kukaa,tuna washukuru walio leta msaada huu na watukumbuke wakati mwingine watuletee hata vitabu na amboksi ya chaki"wamesema wanafunzi hao Yasini na Agnesi.



"Tunawashukuru vijanawetu kwa moyo walio nao tunawaomba na wadau wengine wajitokeze kutusaidia tuna madarasa yetu ni changavu yanahitaji kufanyiwa ukarabati tunaomba mtusaidie "amesema mwenyekiti wa kamati ya Shule Zena Ally.



Kwaupande wake Kaimu Afisa Elimu Msingi na Awali  Selemani Mgeleka amesema kama serikali wapo tayari kushirikiana na wadau hao waelimu na watakapo anza ukarabati wa madarasa hayo watawapa taarifa.


"Napenda kushukuru kwa hichi kikubwa sio kidogo ipo changamoto ya upungufu wa madawati,dawati moja wanakaa wanafunzi watatu akizidi mmoja anakaa chini sisi tunawashukuru kwakuweza kukumbuka mlikotoka naombi lenu tumelipokea kwa mikono miwili lakufanya ukarabati tunawakaribisha ofisi ya elimu shule ya msingi"amesema Mgeleka kaimu afisa elimu msingi na awali.


Akipokea madawati hayo mkuu wa wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva amewashukuru wa wahitimu  hao wakujitolea na kuwaomba wahitimu wengine kujitolea katika shule walizo soma.


"Niwaombe na wahitimu wengine katika shule zao zilizopo manispaa ya Lindi  niwaombe wahitimu walio pita katika shule zetu za Serikali kuiga mfano huu ulio oneshwa na wahitimu wa Shule ya msingi Mitwero.Neno letu kubwa ni asante tunawashukuru sana huu ni wema mkubwa na upendo mkubwa naamini tutaendelea kupokea habari mzuri kama hizi kwa maeneo mengine.Najua mngeweza kufanya mengine lakini mmeamua kufanya hili niseme asanteni sana"amesema Mwanziva mkuu wa wilaya ya Lindi.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI