Header Ads Widget

DC SAME AONYA WANANCHI KUNYWA POMBE MUDA WA KAZI



Na WILLIUM PAUL, SAME. 


MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni ameelezea kukerwa na vitendo vya baadhi ya wananchi kutumia muda mwingi kunywa na kulewa pombe kupitiliza nyakati za kazi hali inayofanya kuwa kero kwa familia zao na jamii inayowazunguka lakini pia kushindwa kufanya kazi za kuwaingizia vipato. 



Ameeleza hayo akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi na baadaye kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi Kata ya Mhezi, ambapo akiwa kwenye mkutano wa hadhara alibaini baadhi ya wananchi walikuwa wamelewa muda wa kazi jambo lililopelekea kupiga marufuku wananchi kulewa muda wa kazi na kuagiza viongozi  wa vijiji na kata wasimamie hilo na kuwachukulia hatua watakao kaidi agizo lake.



“Haiwezekani muda huu wa saa saba mchana watu wamelewa hivi watazalisha na kutunza familia zao saa ngapi….Alihoji Kasilda .



Lakini pia ameagiza viongozi wa Serikali za vijiji kuendelea kufanya msako mkali na kukamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watu wote wanaoendelea kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa maadili ikiwemo kuhamasisha mapenzi na ndoa za jinsia moja (USHOGA) na vitendo vya ulawiti kwa watoto lengo ni kulinda kizazi ambacho kimeingia kwenye janga la mmomonyoko wa maadili.



Aidha  Kasilda ametembelea na kugagua ujenzi wa mradi wa Tanki la maji, Jengo la Kichomea taka na ujenzi wa vyoo vipya matundu matatu miradi inayotekelezwa na Serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni arobaini na mbili, ikiwa ni sehemu ya uboreshaji wa miundombinu ya Zahanati ya Kituvi.


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI