Header Ads Widget

KUWASA YAWATUNUKU WAFANYAKAZI WAKE KWA UTENDAJI ULIOTUKUKA

Mkurugenzi Mtendaji wa KUWASA,Poas Kilangi ( katikati) akikabidhi zawadi ya baiskeli kwa Yosia Michael, mtumishi wa idara ya ufundi kutokana na utendaji wake bora kwenye mamlaka hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa KUWASA,Poas Kilangi ( kulia) akitoa  zawadi ya mkono wa Eid El Fitr na pasaka kwa wafanyakazi wote wa mamlaka hiyo kama motisha kwa kazi nzuri wanayofanya
Mkurugenzi Mtendaji wa KUWASA,Poas Kilangi ( kushoto) akikabidhi zawadi ya kitenge kwa Aste Kambi ambaye ni Fundi mitambo
  kutokana na utendaji wake bora kwenye mamlaka hiyo

xxxxxxx

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MAMLAKA ya maji safi na usafi wa mazingira Kigoma Ujiji (KUWASA) imetoa zawadi mbalimbali kwa watumishi wake ikiwa ni pongezi kwa wafanyakazi hao na kuwapa motisha kwa kazi nzuri wanayofanya kuwahudumia wananchi.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa KUWASA,Poas Kilangi ameongoza bodi ya wakurugenzi ya mamlaka hiyo kutoa pongezi kwa watumishi hao huku akiwataka watumishi hao kuongeza juhudi katika utendaji wao.

 

Miongoni mwa waliotunukiwa zawadi kwenye hafla hiyo ni pamoja na Yosia Michael, mtumishi wa idara ya ufundi ambaye alipewa zawadi ya Baiskeli na Aste Kambi ambaye ni Fundi mitambo na Paskazi Nyalaja, Meneja Utawala na Rasilimali watu waliotunukiwa zawadi ya vitenge.

 

Aidha katika hafla hiyo Mkurugenzi huyo wa KUWASA alitoa fedha taslimu kwa wafanyakazi wote wa mamlaka hiyo kama zawadi za pasaka na Eid El Fitr akiwashukuru wafanyakazi wote kwa kujitoa kwao na kuonyesha ustadi katika kazi zao.

 

Kwa upande wake Yosia Michael akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi hao wa KUWASA alishukuru kwa zawadi hiyo na kuitaja kuwa chachu ya kuongeza bidii na utayari katika shughuli zao za kila siku.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS