Na Zuhura Zukheri Matukio Daima Media
Familia ya mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa na waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu ,Sera, Utumishi na Uratibu, William Lukuvi, inapitia kipindi cha majonzi kufuatia msiba wa mdogo wake mpendwa Xaviery Lukuvi.
Mwili wa marehemu Xaviery Lukuvi umewasili leo kutoka Dar es Salaam kupitia Uwanja wa Ndege wa Iringa, ambako umepokewa na ndugu wa familia, jamaa wa karibu na baadhi ya viongozi wa serikali na chama.
Baada ya mapokezi hayo, mwili huo umepumzishwa kwa takribani saa tatu katika Hospitali ya Wilaya ya Iringa kwa maandalizi ya mwisho, kabla ya kuanza safari ya kuelekea Idodi, alikozaliwa marehemu.
viongozi mbali mbali wa Iringa wakiwa na mheshimiwa Lukuvi Hospital ya wilaya ya Iringa Frelimo kuchukua mwili wa mdogo wake Lukuvi
Shughuli za mazishi zinatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi katika kijiji cha Mapogoro, nyumbani kwao Waziri Lukuvi, ambapo familia, marafiki na waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali wanatarajiwa kushiriki kutoa heshima za mwisho.
Wakati huo huo waziri mkuu Kassim Majaliwa jana amefika nyumbani kwa mheshimiwa Lukuvi Masaki Dar es Salaam kutoa pole kwa familia
MATUKIO DAIMA MEDIA inatoa pole za dhati kwa Mheshimiwa Lukuvi na familia yote katika kipindi hiki kigumu. Tunawaombea faraja, nguvu na utulivu wa moyo.
0 Comments