Header Ads Widget

MBUNGE KILUMBE NG'ENDA AWATAKA WAUMIN WA KIISLAM KUJIJENGEA UWEZO WA KIUCHUMI

 

Mbunge wa  jimbo la Kigoma Mjini Kilumbe Ng'enda (aliyesimama katikati) akizungumza katika Baraza la Eid Al-Adh'haa lililofanyika viwanja vya Kawawa Ujiji mjini Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigom

MBUNGE wa jimbo la Kigoma Mjini Kilumbe Ng’enda amewataka viongozi na waumini wa kiislam mkoani Kigoma kuanzisha miradi ya kiuchumi ili kuwaingizia kipato na kuondokana na hali ya kipato duni inayowakabili waislam wengi mjini Kigoma.


Ng’enda alisema hayo katika baraza la Eid Al Adh’haa lililofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Kawawa mjini Kigoma ambapo alisema kuwa sehemu kubwa ya waumini wa kiislam katika mji huo hawana shughuli maalum za kuwaingizia kipato Zaidi ya kukaa vijiweni na kufanya mambo ambayo yanarudishaa nyuma hali zao za kiuchumi.


Alibainisha kuwa Baraza Kuu la Waislam mkoani humo limeanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya afya na elimu lakini maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo inaenda taratibu kwa sababu waumini wengi wa kiiislam hawachangii miradi hiyo sababu ya hali duni ya kipato jambo ambalo halina afya katika kuujenga uislam.



Sambamba na hilo Mbunge huyo ametoa shilingi milioni 10 kuzindua mfuko wa kusaidia malipo ya walimu wa dini (walimu wa madrasa) ambao utakuwa unakusanya fedha kutoka sehemu mbalimbali ili fedha hizo ziwezesha kuwalipa walimu hao wa madrasa kwa kazi ya kufundisha dini kwani wengi wao pamoja na kazi kubwa wanayofanya hakuna kipato wanachopata kwa kazi hiyo.

Akizungumza katika baraza hilo la Eid Shekhe wa Mkoa Kigoma, Hassan Kiburwa alisema kuwa madrasa zimekuwa kiungo kikubwa katika kufundisha dini na kuwalea watoto wa kiislam japokuwa wazazi wa watoto wanaosoma kwenye madrasa hizo wamekuwa hawalipi kugharamia elimu hiyo japo wanaiona muhimu.


Katika baraza hilo Shekhe huyo wa mkoa Kigoma aliwataka waumini wa kiislam mkoani Kigoma kujitoa kwa hali na mali kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoanzishwa na BAKWATA kwenye wilaya mbalimbali za mkoa huo kwani pamoja na kuwa miradi hiyo ni ya kutoa huduma lakini pia inaingiza kiwango cha mapato ambacho kinaweza kusaidia shughuli za waislam.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI