Header Ads Widget

CAG:MASHIRIKA YA UMMA 24 YALIOPATA FAIDA MWAKA WA FEDHA 2021/22 YAPATA HASARA 2022/23

Na Hamida Ramadhani Matukio Daima app Dodoma

MDHIBITHI  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG) Charles Kichele amesema ripoti iliowasilishwa Machi 28 , 2024 Kwa Rais Samia Suluhu Hassan imeonesha mashirika ya umma 24 yaliyopata faida au ziada katika mwaka wa fedha 2021/22, yamepata hasara au nakisi katika mwaka wa ukaguzi wa 2022/23  huku Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imeendelea kupata hasara kwa 

miaka sita mfululizo.


 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali amesema kwa mwaka 2022/2023 imeonesha  mashirika ya umma 34 yaliripoti hasara au nakisi kwa miaka miwili mfululizo ambapo Mashirika haya yalijumuisha mashirika yanayojiendesha kibiashara 11 na mashirika yasiyo ya kibiashara 23.


Amesema CAG amesema Mwaka wa fedha wa 2022/23 Kampuni ilipata 

hasara ya shilingi bilioni 56.64, hasara hii imeongezeka ikilinganishwa 

na hasara ya shilingi bilioni 35.23 mwaka wa 2021/22, ATCL imeendelea 

kupata hasara licha ya kuwa inapokea ruzuku kutoka Serikalini.



Mashirika yasiyo ya kibiashara yaliripoti nakisi kutokana na upungufu wa 

fedha kutoka Serikalini na vyanzo mbadala vya mapato. 


 ,"Kwa mfano, mwaka wa fedha 2022/23, ATCL ilipokea ruzuku ya shilingi 

bilioni 31.55 kwa ajili ya kugharamia mishahara ya wafanyakazi, 

mafunzo ya majaribio, na ruzuku ya shilingi bilioni 7.45 kwa ajili ya 

miradi ya maendeleo, "imeeleza ripoti hiyo


 "Sababu zinazopelekea hasara zinajumuisha kuwapo kwa gharama kubwa za uendeshaji wa shughuli za ATCL, pamoja na gharama zisizoepukika 

kama vile gharama za ukodishaji na bima kwa ndege ya Airbus A220 -

300 isiyofanya kazi kutokana na matatizo ya kiufundi kama vile kutu na 

kasoro za injini, " Amesema. 


Amesema Matatizo hayo yamegunduliwa na mtengenezaji wa 

ndege hiyo na yameathiri idadi ya ndege za aina hi kote ulimwenguni.

Kuharibika kwa ndege ya Airbus A220 - 300 kuliathiri mwenendo wa

safari za ndege, hivyo kusababisha ATCL kukosa mapato na kushindwa 

kufidia gharama za kudumu za ndege iliyoharibika. 


Aidha, Serikali imechukua hatua mbalimbali ili kuboresha uendeshaji wa kampuni hii ikiwemo, kuundwa kwa timu ya wataalamu inayofanya tathmini ya 

masuala ya kiufundi ya ndege, kifedha na utendaji wa ATCL katika 

biashara ya usafiri wa anga.


Kampuni ya Mawasiliano ya Tanzania (TTCL) imepata hasara kwa 

miaka miwili mfululizo ambapo Katika mwaka wa fedha wa 2022/23, kampuni 

ilipata hasara ya shilingi milioni 894 ikilinganishwa na hasara ya shilingi 

bilioni 19.23 katika mwaka wa fedha 2021/22 huku sababu ya kupungua kwa hasara hiyo ikitajwa kuwa ni ongezeko la mapato mengineyo kwa shilingi bilioni 8.05. Kwa upande mwingine, kuna kupungua kwa gharama kama vile gharama za mauzo kwa shilingi bilioni 12.58 na gharama za uendeshaji wa mtandao kwa shilingi bilioni 6.22. 


"Haya ni matokeo ya mkakati wa kudhibiti gharama uliotumiwa na TTCL katika mwaka wa fedha wa 2022/23.

Aidha, tarehe 30 Oktoba 2022, Serikali ilitangaza nia ya kuhamisha umiliki wa Mkongo wa Taifa (NICTBB) kwenda Kampuni ya TTCL. Uamuzi 

huu unatarajiwa kuongeza mali za kampuni katika mwaka wa fedha 

2023/24, kwa ongezeko la zaidi ya shilingi bilioni 400 kutokana na 

NICTBB,"inaeleza ripoti


Vilevile ripoti hiyo inaeleza kuwa mapato ya jumla ya kampuni yanatarajiwa 

kuongezeka kwa zaidi ya shilingi bilioni 20 kutokana na NICTBB na kwamba Shirika la Masoko la Kariakoo limepata hasara mfululizo kwa miaka 

miwili iliyopita.


Ripoti inafafanua kuwa Katika mwaka wa fedha wa 2022/23, shirika limepata 

hasara ya shilingi bilioni 41.57, ambayo ni kubwa kuliko hasara ya 

shilingi milioni 517.97 iliyopatikana katika mwaka wa fedha uliopita 

2021/22 sababu kuu ya hasara ni kusitishwa kwa ukusanyaji wa 

mapato katika eneo la soko la Kariakoo.


" Hii ni baada ya tukio la moto 

mwaka 2020 ulioteketeza jengo la soko la Kariakoo ambapo kwa matokeo hayo, shirika lilishindwa kukusanya mapato katika soko kwa ukamilifu kuanzia mwaka wa fedha 2020 hadi Juni 2023 kutokana na kusitishwa kwa shughuli za soko ili kupisha ujenzi wa majengo,. 


Aidha, shirika lilirekodi hasara ya shilingi bilioni 41.25 kutokana na 

kupoteza thamani kwa jengo lililoungua ambapo ni sehemu ya matumizi 

yaliyorekodiwa katika mwaka wa fedha 2022/23,Ukiondoa tukio la moto

la mwaka 2020, ambalo lilisababisha kupungua kwa ukusanyaji wa 

mapato, Serikali imekuwa ikilipa gharama za uendeshaji wa kampuni, 

ikiwa ni pamoja na mishahara ya wafanyakazi na gharama zingine, "inaeleza 


Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya CAG katika mwaka wa fedha 2022/23, Serikali ilitenga shilingi milioni 671.15 

kwa ajili ya mishahara ya wafanyakazi na shilingi milioni 518.68 kwa 

matumizi mengineyo ambapo pamoja na Ruzuku kutoka Serikalini, Shirika la 

Masoko la Kariakoo linaendelea kupata hasara.

 

Kwa upande wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) limepata hasara mfululizo kwa miaka miwili iliyofuatana ambapo Katika mwaka wa fedha 2022/23, shirika lilipata hasara ya shilingi bilioni 100.70, ikilinganishwa na hasara ya shilingi bilioni 190.01 katika mwaka wa fedha 2021/22.Aidha Shirika limeendelea kupata hasara licha ya kuwa linapokea ruzuku kutoka Serikalini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS