Header Ads Widget

RC KUNENGE APOKEA TANI 300 ZA CHAKULA KUTOKA KWA RAIS DKT SAMIA YEYE BINAFSI KWAAJILI YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI

 

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amepokea msaada wa mchele, Maharage na unga tani 300 kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan yeye binafsi kwaajili ya waathirika wa mafuriko  yanayoendelea katika Mto Rufiji kwa Wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani msaada uliowakirishwa na Innocent Mbilinyi.


Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Ikwiriri Wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati wa kupokea msaada huo Kunenge ameshukuru kwa misaada huo ambapo tayari tani 32 za mchele zimekwisha wasili na kupokelewa wilayani Rufiji huku tani zingine zikiwa Barabarani kuletwa wilayani humo.


Kunenge alisema Mheshimiwa Rais amekuwa akiwapelekea misaada mingi ya aina mbalimbali kwaajili ya Wananchi wa mkoa huo wanapopatwa na maafa mbalimbali kutoka serikalini lakini msaada huu wa tani 300 ni msaada alioutoa yeye binafsi.


"Mheshimiwa Rais amekuwa akituletea misaada mingi kutoka serikalini lakini msaada huu ametoa yeye binafsi na sisi tunaahidi tutaigawa misaada hii kwa kusimamia vizuri kwa walengwa kama ambavyo yeye imempendeza kutoa msaada huu" alisema Kunenge.


"Lakini nimshukuru Mbunge wa jimbo la Rufiji na Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa kwa Kazi kubwa anayoifanya ya kututafutia misaada mbalimbali na sisi tumuahidi kwamba misaada yote inayokuja tutaisimamia vizuri kwa kutumiwa na walengwa kama ilivyokusudiwa" alisema Kunenge.


Naye Innocent Mbilinyi alikabidhi msaada huo kwaniaba ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Msaada huo wa mchele daraja la kwanza tani 100, maharage tani 100 na unga tani 100 ambapo tani zilizofika tayari ni tani 32 wakati tani zingine zikiendelea kuja.


Na baada ya kukabidhiwa alikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele kwaajili ya usambazaji kwa walengwa waathirika wa mafuriko katika Wilaya za Kibiti na Rufiji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS