Header Ads Widget

ASILIMIA 80 YA WATANZANIA KUTUMIA GESI IFIKAPO 2034

 





Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma


NAIBU Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amesema hadi kufikia mwaka 2034 asimia 80 ya watanzani watakuwa wanatumia Nishati ya gesi ya kupikia majumbani


Hayo ameyasemwa leo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa 13 wa Kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa mwaka 2024 ambapo amesema Nyote mnafahamu kuwa dunia imemchagua Rais Samia kuwa Kinara wa uhamasishaji matumizi ya Nishati safi ya kupikia, ambayo ni gesi kwa Bara la Afrika. 


Amesema Kwa mabara mengine kama Ulaya, Amerika ya Kusini na Kaskazini na Asia, kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia nishati ya gesi kwa ajili ya kupikia majumbani. Kwa mabara haya, kukata mti kwa ajili ya kuni au mkaa inachukuliwa kuwa ni uhalifu usiokubalika.


Nchi za wenzetu wanatumia gesi kwa ajili ya kupikia, mfumo wa joto katika nyumba zao katika kipindi cha majira ya baridi, na kama Mwenyekiti alivyosema, gesi inatumika sasa kuendeshea magari. Sisi kama Wizara ya Nishati tumeandaa mpango kabambe wa kuhamasisha matumizi ya gesi hapa nchini.


"Wakati Rais wetu, Mama Samia anakwenda katika nchi nyingine za Afrika kuhamasisha matumizi ya gesi, sisi tumesema nchi hizo zije kujifunza hapa kwetu Tayari tunao mpango na tumeanza kusambaza mitungi ya gesi hadi vijijini, ambako tunataka mama wa kijijini atumie gesi aachane kabisa na mahangaiko ya kutafuta kuni, ".


Na kuongeza"Tunafahamu katika baadhi ya mikoa, moshi unaotokana na kuni umekuwa chanzo cha mauaji kwa akina mama wazee wanaokuwa na macho mekundu kwa sababu ya moshi huo wakituhumiwa uchawi Sisi tunaamini tukimuunga mkono vyema Rais Samia tukahamasisha matumizi ya gesi vizuri, watu wetu watapata faida kubwa.


Amesema Zipo faida nyingi unapotumia gesi, ambazo kati yake kubwa ni ulinzi wa misitu yetu na hivyo kuliepusha taifa na dunia na hatari ya jangwa. Tunapokata misitu, tunaharibu ardhi. Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 16 ya ardhi ya nchi yetu imeharibiwa kutokana na ukataji miti holela.


Aidha amesema Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira nchini ya Mwaka 2019, inaonesha kuwa kasi ya uharibifu wa misitu ni kubwa na kila mwaka zaidi ya hekta 469,420 huharibiwa kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa.


 Ameeleza Hadi kufikia 2015, uzalishaji wa mkaa duniani ulikadiriwa kuwa tani milioni 52 kwa mwaka, na kati ya hizo tani milioni 32.4 zinazalishwa Afrika, ambapo asilimia 42 ya tani hizo zinazalishwa katika ukanda wa Afrika Mashariki unaohusisha nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi. 


Amesema afrika Magharibi inazalisha asilimia 32, Afrika ya Kati (12.2), Kaskazini (9.8) na Kusini mwa Afrika ni asilimia 3.4.


Amesema Takwimu hizio  zinaashiria hatari kubwa kuwa Misitu inateketea katika ukanda wetu. Wahariri fanyeni jambo Ungeni mkono juhudi za serikali, vinginevyo kama tusipofanya kitu, nchi yetu itageuka jangwa si muda mrefu na kwa hakika sisi kama Serikali, hatutakubali hili litokee.


Amesema Katika Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDG) ya Mwaka 2030, Lengo Na. 7 linaelekeza upatikanaji wa nishati safi na ya bei nafuu. 


"Sisi hapa Tanzania tumebahatika kuwa na gesi ya kutosha na Ndiyo maana  Rais Samia amesema tuitumie gesi hii, ambayo ina bei nafuu tuokoe misitu na maisha ya kina mama huko vijijini, " Amesema.


Na kuongeza "Hili la kutumia gesi kama nishati ya kuendeshea magari, sisi kama Wizara tunalipa msukumo mkubwa na Tunajipnaga kujenga vituo vikukbwa vya kusambaza gesi ya magari na Kanuni imeruhusu sasa wenye vituo vya mafuta vya kawaida kuongeza uuzaji wa gesi, hii tukiamini itasaidia kuongeza kasi ya kusambaza gesi ya magari nchini, " .


Mkutano wa Kitaaluma Kila Mwaka


Aidha mewataka Mkutano huo wautumie kuona kama taaluma iko sawa sawa au nanyi mmepata wavamizi wanaoitwa ‘Makanjanja’. Kuna watu wanajipachika uandishi wa habari huko, wanapiga simu kwa watu mbalimbali na kudai fedha kwa vitisho kuwa wasipopewa wanawalipua. Hili nalo mliangalie linaharibu taswira nzuri ya taaluma yenu.


"Mmetaja hapa mitandao ya kijamii, kuwa inatumika vibaya na kuna uwezekano wa kuwapa mafunzo wahusika wakawa watoa taarifa wazuri kwa kufuata misingi ya kitaaluma. Sisi tunasema leteni hayo mapendekezo jinsi mtakavyoifanya kazi hii, na pale tulipo na uwezo tutaona jinsi ya kusaidiana kwa nia ya kukuza taaluma hii muhimu.


Na kuongeza "Jambo la msingi katika kikao hiki mchekeche kweli kweli misingi ya taaluma, matakwa ya kisheria, maadili yetu katika jamii kama nchi, misingi taifa letu, umoja wetu, kuulinda Muungano wetu, kuendeleza siasa za kistaarabu, rasilimali za umma - kumulika kama wahusika wanazisimamia vizuri, bila kusahau kama nilivyosema ninyi wenyewe kujimulika iwapo mnaifanya kazi ya uhariri na uandishi wa habari kama inavyostahili.


Kwa hali yoyote iwayo, kimsingi mimi nawapongeza kwa mkutano huu mzuri na natarajia kupitia maazimio mtakayoyafikia, basi mtatushirikisha kama Serikali tuone wapi tunaweza kuchangia nini kufanikisha taaluma yenu ya habari ikawa bora zaidi.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Deodatus Balile amesema kuwa wamebaini kuwapo kwa dalili za rasilimali ya gesi kutotumika ipasavyo kutatua changamoto hasa katika sekta ya nishati, kwa maana ya upatikanaji wa umeme nchini na kutumiwa kama nishati safi ya kupikia kwa akina mama, licha ya kujengwa bomba la kusafirisha rasilimali hiyo kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, ambalo ujenzi wake uligharimu mabilioni ya shilingi za Kitanzania.


"Bomba hili kwa taarifa tulizonazo linatumika kwa kiwango cha chini kwani miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi pale Kenyerezi, Dar es Salaam haijafanya kazi kwa idadi ya megawati zilizokusudiwa ," Amesema


Na kuongeza " Tuliahidiwa Kinyerezi I, II, III na IV, lakini taarifa tulizonazo, Kinyerezi III na IV hazijafanya kazi kwa kiwango kilichokusudiwa, ".


Amesema hapo mwanzo tulielezwa kuwa nyumba nyingi za watu binafsi zingeunganishwa katika mfumo wa gesi asilia na kutumia nishati hii kupikia ambayo ina nafuu kubwa ikilinganishwa na nishati nyingine. 


Amesema Tuliaminishwa kuwa vituo vya mafuta nchini vingeunganishwa na nishati hii ya gesi asilia, ambapo gharama ya kuendesha magari kwa kutumia gesi ni ya chini mno. 


"Mfano wakati mtumiaji wa gari dogo la IST anajaza mafuta lita 40 kwa wastani wa Sh 120,000, kwa umbali ule ule anayetumia gesi anajaza mtungi mmoja kwa Sh 17,000. Dar es Salaam sasa ina vituo vitatu vya kesi na Dangote anacho kimoja mkoani Mtwara na mikoa mingine yote nchini haina kituo hata kimoja, " Amesema Mwenyekiti huyo .


Na kuongeza " Sisi Wahariri, tunatamani kuona mchango wa rasilimali gesi katika uchumi wa nchi yetu na watu wake, na zaidi kusaidia taifa kuondokana na changamoto ya akina mama wenye macho mekundu kutokana na moshi wa kuni kudhaniwa kuwa ni wachawi na kuuawa katika baadhi ya mikoa hapa nchini, " Amesema


Kwa upande wake Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema taarifa kuhusu uchumi wa vyombo vya habari imekamilika na wanatarajia kumkabidhi  Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan


Amesema Kamati ambayo ili kuwa ikikusanya taarifa imefanya kazi kubwa na imekamilisha kazi hiyo kwa umakini makubwa


Hata hivyo amemuomba Naibu Waziri Mkuu kutilia mkazo suala la madeni ya vyombo vya habari ili yalipwe na baadhi ya Taasisi na Serikali na Halmashauri ili kuvinusuru Vyombo vya Habari visife. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS