Header Ads Widget

MAKALA AONYA WANASIASA WACHOCHEZI

 


CHAMA cha Mapinduzi (CCM )kimewaonya baadhi ya wanasiasa wanaoendesha harakati  zao za kisiasa kwa kujaribu kutoa kauli za kichochezi  kuacha kufanya hivyo mara moja na waendeshe siasa za ustaraabu.


Hayo yamesemwa  leo Aprili 29,2024 jijini Dodoma  na Katibu wa Nec  Itikadi  Uenezi na Mafunzo  (NEC ) Amos Makalla wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema amesikitishwa na kauli  zilizotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA) Tundu Lisu  wakati akiwahutubia wananchi waliofika kwenye maandamano yao leo jijini Dodoma.


"Lisu ametumia maneno ya kibaguzi kwamba Rais samia ni Mzanzibar  na isingekuwa Muungano hana Mamlaka ya kuhamisha watu waliopo Ngorongoro  huyu ni Mzanzibar  akaenda mbali zaidi akisema  anayafanya haya kwasababu ni Mzanzbar"amesema Makalla

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS