WANANCHI wa Igoda kata ya Luhunga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamefutahishwa na ziara ya mkuu wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba kuwa ameweza kushuhudia kero ya barabara ya Mafinga -Sawala.
Wakizungumza na Matukio Daima media leo wananchi hao wamesema pamoja na kuwa leo hakuna mvua ila kwa sehemu ataona changamoto ya ubovu wa barabara kuu ya Mafinga -Sawala hadi Mgololo.
Walisema kero ya ubovu wa barabara hiyo ni Mateso makubwa kwa wananchi pia ni hatari kwa ukuaji wa uchumi wa wilaya ya Mufindi.
0 Comments