Header Ads Widget

MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UJENZI WA SOKO LA MACHINGA NA UWANJA


Na,Jusline Marco:Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameshuhudia hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa soko la machinga eneo la Morombo na uwanja wa mpira wa Arusha City Club katika kata ya Murieti, Jiji la Arusha.

Makonda ameeleza kuwa miradi hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM na jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akibainisha kuwa fedha za ujenzi wa soko hilo zilitengwa tangu mwaka 2021 na ni fedha za serikali kuu, siyo halmashauri.

“Niliwaambia viongozi wa Jiji la Arusha, huu mwaka ukiisha soko halijajengwa, basi ama zao ama zangu. Leo nimefika hapa kushuhudia hatua hii muhimu mbele ya wananchi na tunataka miradi yote yenye fedha tayari itekelezwe kabla ya mwezi Julai ili wananchi waanze kunufaika,” amesisitiza Makonda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, John Kayombo, amesema uwanja huo utajengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 9.6 na utakuwa na uwezo wa kubeba watazamaji 8,000 waliokaa. Pia utajumuisha viwanja vidogo vitatu vya mpira wa pete, mpira wa kikapu na tenisi na utatekelezwa na kampuni ya STC Construction Company Ltd na unalenga kuinua vipaji na kuongeza mapato kwa Jiji la Arusha.

Mradi wa ujenzi wa soko la machinga unatekelezwa na kampuni ya SUMA JKT Construction Company Ltd kwa gharama ya Shilingi milioni 710.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI