Na Esther Machangu Matukio Daima Moshi.
Wadau wa vyanzo vya Maji na utunzaji wa Mazingira wamekabidhi taarifa za ubora wa Maji kwa Mamlaka ya Maji bonde la Mto pangani Ili kuwahakikishi watumiaji wa Maji wa Maji wa vijiji sita vya Uru kusini na Uru kaskazini, wanatumia rasilimali hiyo bila kuhofia kupata magonjwa yalipuko
Wakiongea wakati wa kukabidhi Ripoti hiyo Desemba 6,2023 katika ofisin za Bonge la Mto pangani, wamebainisha kuwa hapo awali Maji hayo hayakuwa yemepimwa na walipewa ushauri na Viongozi wa Bonde la Mto pangani kufuata taratibu za kwenda kuyapima Maji hayo Ili kujihakikishia usalama zaidi.
Mmoja wa wadau hao Michael Kimath amesema kuwa maboresho yaliyofanyika katika chechem hizo za,Mboriko,Owa,Mbora,Mkomboni, ni pamoja na kujenga Banio la Maji Ili kuyalinda yasiweze kuchafuliwa.
Aidha ameongeza kuwa Mwananchi na Mkoa wa Kilimanjaro hawana budi kuyatunza Mazingira kwani ndio chanzo kikuu kinachofanya chemchem hizo ziendelee kuwepo vizazi hadi vizazi
Mjumbe kutoka Jumuiya ya Chioloka kata ya Uru kusini Livin Mushi (Mc JB) amesema, wamefanikiwa kufikia malengo hayo kutokana na ubora wa ujenzi katika chemchem hizo na pia ushirikishwaji wa Malamka ya Maji ya Bonde la pangani pamoja na Wananchi wanaoishi pembezoni mwa vyanzo hivyo.
Kwa upande wake Christopher Kisarika katibu wa Chanzo Cha Maji Cha chemchem ya mkomboni Water Trust, amesema katika kipindi hiki Cha kuelekea mwishoni mwa Mwaka wageni wote wanaokuja katika Mji wa Moshi hasa katika kata za Uru Kusini na Uru kaskazini wawe huru kufungua Maji katika mabomba ya kunywa kwani Maji hayo yameshadhibitishwa ubora wake na Mamlaka husika kuwa ni Safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Hata hivyo wametoa Shukrani zao kwa mdau wa maendeleo na wa kata hiyo Lenard Kisarika kwa kujitoa kwake Ili kuhakikisha vibali vya matumizi hayo ya Maji vinapatika Ili kuondoa hofu Kwa jamii inayotumika Maji hayo.
Mwisho
0 Comments