Header Ads Widget

WALIMU WAASWA KUTOSHIRIKI UKUSANYAJI WA MICHANGO SHULENI,ILI KUEPUKA MIGOGORO BAINA YAO NA WAZAZI.

Na Shemsa Mussa,Kagera.

Katika kuendeleza Sera ya Elimu bila Malipo Walimu watakiwa kutokujihusisha na michango mbalimbali ya  shule inayotolewa na wazazi ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza.


Rai hiyo imetolewa na Afsa elimu Awali na Msingi Manispaa ya Bukoba,  Mwalimu Baseki Sheja alipokuwa ofisini kwake,ambapo amesema kuwa katika suala la michango shuleni lina utaratibu wake ambapo amesema wananchi wanatakiwa kukaa kikao kujadili na kukubaliana wao wenyewe na kupata kibari kutoka ngazi ya juu na baadae kuanza kuchangia kitu fulani bila kuwashirikisha walimu.


"Asilimia kubwa ya walimu katika shule zetu wanawapenda sana wanafunzi wao kwa hiyo na wanapenda wapate huduma zote hasa chakula hivyo ikitokea kuna baadhi ya michango wanatoa hata wao ni jambo jema na ni upendo na tunapaswa tuwashukuru sana pia nao ni wazazi na ni ushirikiano tunaotaka ila sio wao kuwa waratibu,acha wazazi wachaguane wao mwalimu ukitaka kushiriki shiriki kama mzazi,amesema Mwalimu Sheja"


Aidha, Bw Sheja ameendelea kusisitiza kuwa  katika zoezi hilo la kuchangia maendeleo ya shule hapatakiwi kumuhusisha mwanafunzi na kukwamisha masomo yake huku akusema jukumu la mwanafunzi ni kusoma sio kushiriki katika michango na pia mwalimu atakayebainika akijishughulisha na jambo hilo sheria kali zitachukuliwa dhidi yake.


Amesema katika suala la Elimu Msingi bila Malipo ni moja ya njia ya kupate elimu bila kulipia huku ikiwa na maana ya mzazi akimpeleka mtoto  kumwandikisha masomo asitozwe au kudaiwa chochote huku akisema hakuna suala la toa kiasi kadhaa upate elimu ikiwa jitihada zote hizo zinahitaji ushirikiano  kwa wadau wa elimu huku serikali ikiwa mdau mkubwa wa jambo hilo.

Pia amewasisitiza wazazi kuendelea kutoa ushirikiano  hasa katika kuwahudumia watoto wao katika suala la kupata elimu na hasa kuchangia huduma ya uji au chakula ili watoto wawapo shuleni waweze kupata huduma ya chakula na kusema kuwa chakula sio mchango bali ni haki ya mtoto ,akiwa nyumbani lazma apate chakula hivyo hivyo awapo shule lazima aweze kula .


Amesema katika suala la elimu bila malipo kuna changamoto ya baadhi ya wazazi kujiaminisha kuwa hatakiwi kughalamaia chochote kwenye harakati  za elimu ambapo kuna miongozo inayoeleza wajibu wa mzazi na wajibu wa serikali lakini baadhi ya wazazi wamekuwa wagumu kwenye hilo .


Katika kukabiliana na michango inayotozwa bila mpangilio kwenye baadhi ya shule Mtandao wa kijamii wa (jamiiforums) hivi karibuni ulirusha taarifa kutoka kwa Mdau wa elimu ikieleza namna Wazazi wa Wanafunzi wa Shule ya sekondari Bujunangoma  iliyopo katika kata katerero ndani ya Halmashauri ya Bukoba wanavyokerwa na wingi wa Michango .


Mdau huyo ameeleza  kuwa shule hiyo imekumbwa na orodha ndefu ya michango inayochangwa shuleni hapo kiasi cha kusababisha mpaka baadhi ya wahitimu kushindwa kupata vyeti vyao (Leaving Certificate) pindi wanapohitimu na wengine kupata bila kusainiwa ,na mara nyingi wamakuwa wakilazimishwa kulipa fedha taslimu (mkononi) na inapolipwa fedha hiyo hawapewi risiti ili kujua na kutambua ni wapi fedha hizo zinakwenda.


Mdau amesema michango wanayolazimishwa kulipia ni kama Mche wa Mti,Jezi ,Ujenzi wa choo ,karatasi  za kusomea ,Ndoo kubwa  pamoja na kitabu kinachodaiwa kupotea.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI