Na Pamela Mollel,Arusha
Waziri wa Maliasili na utalii Angela Kairuki amepongeza TAWIRI Kwa kufanya makongamano hayo ya kisayansi kila mwaka ambapo Washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi 22 wamejitokeza katika kongamano Hilo la wazawa la takribani siku 3.
Akizungumza na waandishi wa habari mhe waziri amesema kuwa serikali na taasisi zake imekuwa ikitumika matokeo ya tafiti zao pamoja na mapendekezo.
Alisema kuwa mada kubwa katika kongamano hilo ni mwingiliano kati ya wanyamapori na binadamu ambapo eneo kubwa Kuna uwepo wa changamoto katika wilaya 81 kati yake 44 zikiwa kwenye ndio zimekithiri zaidi ambapo kupitia matokeo hayo ya uchafuzi kama wizara wameandaa mpango wa namna ya kukabiliana na Changamoto hizo Kwa kuweka matumizi ya teknolojia Kwa kufunga Kola katika baadhi ya Tembo,Simba na wanyama wengine.
Aidha maeneo ambayo tayari yamewekwa kola ni pamoja na Serengeti,Mikumi,Mkomanzi ambapo kupitia tafiti za Tawiri imebainika wakati wa kiangazi Tembo na wanyama wengine wanasemekana huingia sana kwenye maeneo ya watu kutoka km 5 mahali watu wamejenga makazi ndio maana husikia watu wengi wameuliwa sana.
Serikali imejipanga kujenga mabwawa mengi ya maji kama njia ya kuwasaidia wanyama wakati wa kiangazi kupata maji ambapo wamefanya hivyo eneo la mkomazi na maeneo mengine ambapo serikali inaendelea kupanga bajeti ili kuhakikisha watu wanakuwa salama na kuwasaidia wanyama.
Kadhalika serikali imekuja na teknolojia mpya ya fensi ya kisasa ambapo inaweza kuwekwa katika mpaka wa Hifadhi ambao huu utasidia kuwapa ishara na alamu il kuwasaidia askari wa wanyama pori kutatua changamoto Kwa wakati.
Waziri Kairuki amesema kuwa serikali haipendelei kuona wafugaji kuingiza mifugo ndani ya hifadhi kwani maeneo hayo yanahitajika kutunza ipasavyo hivyo Amewaasa jamii za kifugaji kuepuka kuingiza mifugo
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa wanyama pori Tanzania (TAWIRI) Dr Ernest Mjingo amesema kuwa lengo la kongamano Hilo ni kusambaza matokeo ya tafiti zilizokwisha kufanyika tayari
Alisema kuwa usiposambaza tafiti ambazo zilikwisha kufanyika zinakuwa hazina maana ambapo katika ukumbi wa mikutano wa Aicc Leo mataifa zaidi ya 22 yamekutana ambapo lengo kubwa ni kubadilishana taaluma na matokeo ya kitafiti yaliyofanyika miaka 2 iliyopita .
Dr Mjingo amesema kuwa tafiti hizo ndizo zinasaidia uhifadhi na kuendeleza utalii kwani matokeo hayo hutumika kutengeneza elimu za uhifadhi.
Kwa upande wao baadhi ya watafiti na wadau walioshiriki katika kongamano la 14 la TAWIRI akiwemo Kipemba Ntiniwa kutoka taasisi ya TAWIRI amesema kuwa wamekuwa na bidhaa zitokanazo na Mazao ya nyuki kama vile Asali,Nta na bidhaa zinginezo lengo likiwa ni kuonyesha watanzania umuhimu wa nyuki.
Aidha Ntiniwa amesema kuwa zipo bidhaa zimeongezewa thamani kutokana na Mazao ya nyuki ili yaweze kuuzwa Kwa bei kubwa na kuongeza kipato Kwa watu kama vile dawa za ngozi,mishumaa,mafuta ya kujipaka, za dawa za kuchua.
Pia amesema kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kutengeneza mshumaa maalum wa kuondoa msongo wa mawazo kutokana na kutengenezwa kitaalam na mchanganyiko wa manukato mbalimbali ambao pia una uwezo wa kuangamiza wadudu mbalimbali kama vile mbu,nzi na wengineyo.
John Itembe meneja msaidizi wa katika kampuni ya TNC mkoani Arusha wakati akizungumza katika kongamano Hilo amesema kuwa TNC ni taasis inayofanya kazi katika nchi 70 duniani na nchi 9 afrika ambapo makao makuu yapo Arusha Tanzania ambapo taasis hiyo inashughilika na masuala ya uhifadhi na mazingira pamoja na kuhudumia Taasis za ndani.
Kwa upande wake mratibu wa nyanda za malusho Paulo Loshilo katika kongamano Hilo amesema kuwa wamekujaa kutoa elimu ya malisho Kwa wafugaji katika kongamano hilo dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi namna ambavyo wanatumia mbinu za kisasa ambapo wamekiri kufanikiwa Kwa asilimia 60.
0 Comments