Na Pamela Mollel, Monduli.
Afisa mtendaji mkuu wa benki ya uchumi kanda ya kaskazini Samweli Wado amewasisitiza wahitimu wa kidato Cha 4 nchini kujipanga kimasomo kwani elimu waliyoipata ni ndogo kutokana na ongezeko kubwa la teknolojia ambapo aliipongeza taasisi ya elimu ya Tumaini Kwa kutangulia kufanyia kazi mtaala mpya wa elimu.
Alisema kuwa anapongeza shule hii Kwa kufanya vizuri kitaaluma ikiwemo kufuata nyendo za serikali kielimu hususani katika mtaala.mpya kwani Wahitimu wa kidato Cha 4 wameonesha mambo mazito ambayo ndio mpango halisi wa serikali kitaaluma kutokana na uelewa mkubwa.
Kadhalika Afisa mtendaji huyo wakati akizungumza katika Mahafali hayo ya 5 ya kidato Cha 4 ya shule ya sekondari Tumaini Senior aliwasisitiza wazazi kuendelea kuwawekea watoto wao akiba katika taasis ya kifedha ya uchumi kama njia mojawapo ya kujipanga kuwaendeleza watoto Hadi vyuo vikuu.
Pia aliwataka wanafunzi kufahamu umuhimu wa kujiwekea akiba katika maisha yao kwani ni faida kubwa na kufahamu nidhamu ya kutunza fedha, ambapo aliwapongeza Wahitimu Kwa kuonyesha Kwa vitendo yale waliojifunza zikiwemo tafiti mbalimbali za kuisaidia jamii ya kitanzania.
Aliwataka wazazi kuendelea kushirikiana na waalimu katika kuendeleza vipaji vya watoto na kuwatia moyo Kila mara kwani vipaji ni ajira ikiwemo kuhakikisha watoto wanakulua maadili mema.
Aliwapongeza Wahitimu kidato Cha nne na kuwaasa kutambua elimu waliyo nayo namna inaweza kuwapa nguvu na kuhakikisha wanakuwa chachu katika jamii Kwa kuyafanyia yale walizojifunza kipindi wakiwa shuleni zaidi.
Aidha aliwaasa wahitimu hao kuwa watu wa malengo Kwa kujituma na kujitoa zaidi katuka shughuli mbalimbali za kijamii na kifamilia ili kuwajengea uwezo na kuhakikisha wanaitumia elimu yao ilasavyo.
Tumieni changamoto kama fursa na kubakia kihalisia zaidi na haikikisha Kila siku unaongeza kitu kipya ili kukua kuelekea katika mafanikio Yako.
Aliwaasa kumtanguliza Mungu mbele na kuendelea iumtegemea Mungu kama ambavyo maandiko matakatifu yanavyoelekeza.
Pia alisema kuwa nidhamu ipewe kipaumbele ili uweze kuona matunda yako ni kulingana na Muda uliokuwa ukijituma ma tambua ndio mafanikio yako.
Alisema bado wazazi wanalo jukumu la kuendelea kuwainua watoto kwa kuwaandaa vizuri kwa kuwapa elimu Bora kwani ndio urithi wa kweli
Aliwashukuru waalimu Kwa kuwapatia maarifa mazuri ambapo aliwaasa wazazi kwenda kuwaandikisha watoto kwa wingi Tumain Senior kwani shule hiyo inajali masilahi ya watoto .
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi za elimu Tumain Modest Bayo aliwataka Wahitimu kujipanga kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano kwani bado hawajakamiliaha ndoto zao kufuatia watoto hao kuhitajika kusoma mpaka elimu ya vyuo vikuu.
Aidha Wahitimu wa kidato Cha nne wamethibitisha namna ambavyo shule ya Tumain Senior inawanoa wanafunzi kitaaluma na kimaadili.
Kadhalika mkurugenzi huyo aliwaasa wazazi kuendelea kutoa ushirikiano Kwa waalimu ili kuwasaidia watoto wazidi kufanya vizuri katika masomo yao.
Alisema kuwa shule ipo katika mikono salama na pia kuhusiana na mtaala mpya utalenga zaidi kumsaidia mwanafunzi kujitegemea badala ya kuwa tegemezi ambapo mwanafunzi atanufaika na masomo kulingana na mazingira ikiwa mwanafunzi Anatoka katika jamii ja kifugaji basi atafundishwa hivyo na ikiwa Anatoka katika maeneo ya kilimo basi afanye kilimo cha kisasa zaidi.
Kwa upande wa Taasis za elimu ipo miradi mbalimbali ikiwemo masomo ya mziki yaliyopo kwenye somo la PBL na ambapo aliwataka wazazi kuendelea kuwaamini.
Tumaini inategemewa kuwa shule ya kwaza kuunga mkono mtaala mpya kwani tayari walishaanza mapema hivyo wazazi waendelee kuwaandikisha wanafunzi katika shule za Tumaini.
Akizungumzia uboreshaji afya za wanafunzi katika shule za Tumaini Bwana Bayo alisema kuwa hali ya chakula shuleni ipo vizuri kwani nyama na mboga za majani ni kipaumbele Kwa wanafunzi
Hata hivyo katika kutatua changamoto ya uhaba wa maji shule wazazi Kwa kushirikiana na taasis mbalimbali ambao ni marafiki wameweza kupata zaidi milioni mbili huku mahitaji yakiwa ni milioni 3 lengo ni kuhakikisha huduma za maji zinakuwepo wakati wote.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo ya Tumaini senior Sifael Martin Msengu amesema kuwa katika Mahafali hayo ya 5jumla ya Wahitimu 45 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya kidato Cha 4.
Alisema kuwa kuhusiana na mtaala mpya tayari Wana uzoefu wa miaka 7 na endapo vyeti vitatolewa shule za Tumaini watapatiwa vyeti mara mbili ambapo alisema kuwa katika shule hiyo wanafunzi huwezeshwa sana Kwa kudadisi vipaji vya watoto na kuvipa kipaumbele.
Hata hivyo Wanafunzi waliohitimu kidato 4 walitoa zawadi ya waalimu wao kutokana na kuwafunza vema ambapo mkuu wa shule alipatiwa Kombe Kwa kuwapigania kipindi Cha elimu.
0 Comments