CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMAAPP MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla amewataka Wakuu wa wilaya mkoani humo kuunda kamati na kufanya mikutano ya kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara kabla ya mwezi disemba mwaka huu kuisha.
Maagizo hayo ameyatoa wakati akisikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara walizonazo ikiwa ni katika kuhakikisha wanaboresha biashara zao pamoja na kuweka uelewa wa pamoja.
Makalla amewataka watendaji kila sekta kuangalia tozo zilizopo zi wafabyabiashara badala ya kuwainua zikiwe pia ushuru wa huduma ili kutoka na pendekezo la namna ya kuboresha na kuondoa sintofahamu hizo hususani utitiri wa tozo huku zingine zikionekana kujirudia baina ya taasisi.
"Watendaji wa Mamlaka ya Mapato na na maafisa biashara tuwe na lugha nzuri ya kudai kodi na kuwatia moyo watu ili wafanye biashara maana serikali inaweka mipango mbalimbali ya kuboresha huduma za jamii kwa kutumua kodi hivyo ni lazima tutengeneze mahusiano mazuri na wafanya biashara na sio kuwakatisha tamaa." Alisema Makalla.
Makalla amekuwa katika kushughulikia adhabu za makosa ya maegesho, ni lazima kuwekwa kwa vibao vitakavyosaidia kuonesha sehemu zinazorubusiwa au kukatazwa kuegesha badala ya kusubiri watumiaji wa barabara wafanye makosa ili wawatoze faini.
"Huu ni uzembe, na tabia ya watu kupandilia Sheria, nataka operesheni ya kusimamia sheria ili daladala, bodaboda na bajaji zifuate taratibu zitakazoeleweka nawaagiza wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na LATRA kwenda kushirikiana kuondoa changamoto" Amesema Makalla.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara, Mwenyekiti wa chemba Gabriel Chacha ameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na utitiri wa Kodi, tozo, ushuru na leseni kinzani kwenye utoaji wa huduma na mamlaka za serikali kuingiliana kwenye utozaji kwenye mambo yanayofanana.
"Tunashinda kufanya kazi kutokana na tozo kuwa nyingi na biashara zetu hazikui wakati mwingine Tra kufunga mirango ya wafanyabiashara kutokana na kuchelewa kukupa Kodi" Alisema Gabriel.
0 Comments